Search This Blog

Saturday, September 22, 2012

OFFICIAL: YANGA YAMTIMUA KOCHA TOM SAINTFIET

Wote wametimuliwa Yanga
Fukuza fukuza ya klabu ya Yanga iliyoanza leo mchana baada ya mkutano wa wajumbe wa kamati ya utendaji uliofanyika leo katika makao makuu ya klabu imeendelea imemkumbuka kocha mkuu wa klabu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet.

Taarifa za uhakika kutoka kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ni kwamba  uongozi wa timu hiyo umefikia maamuzi ya kumtimua kazi kocha huyo aliyeajiriwa miezi mitatu iliyopita kutokana na kutofautiana sera za namna ya kuiendesha klabu na uongozi wa juu wa mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati.

Mchana leo kamati ya utendaji ilisimamisha ajira za viongozi waajiriwa wote wa klabu hiyo akiwemo katibu mkuu Celestine Mwesigwa na msemaji Luis Sendeu huku ikitoa onyo kwa kocha Saintfiet kwa tabia yake ya kuongea na waandishi wa habari bila mpangilio wa klabu. Lakini baada ya taarifa hizo kutoka usiku wa leo kocha huyo akaonekana akiongea kwenye television mojawapo nchini akizungumzia mambo mbalimbali kuihusu Yanga.

Kwa mujibu wa Sanga anasema kwamba sakata lote la jinsi kocha huyo alivyopoteza kazi yake litatolewa ufafanuzi hapo kesho.

Wakati huo huo aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga kabla ya Mwesigwa, Lawrence Mwalusako amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo ya ukatibu mkuu wa Yanga kwa muda, wakati mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Seikolojo Chambua amekabidhiwa majukumu ya kuwa meneja wa timu hiyo akichukua nafasi ya Hafidh Salehe ambaye nae aliondolewa leo mchana.

Nafasi ya usemaji wa Yanga mpaka sasa imekuwa kitendawili, tetesi zinasema kuwa mtangazaji wa Clouds FM NA Clouds TV Abdul Mohamed na Mwanahabari Mahmoud Zubeiry mmojawapo anaweza kula shavu la kumrithi Sendeu.

1 comment:

  1. mimi ni mmoja kati ya watu ambao nimeiona yanga ktk mechi zote kuanzia kagame mpaka friends match, hii tem haiko vizuri kitambo kama hawaamini watafute review za hizo mechi uone kama yanga walikuwa wana move yoyote kuelekea kutafuta goli,, yani zero kabisa na tukasema hii team ina focus kupata kitita cha kagame na si team nzuri kwa ligi,,
    leo yameonekana check zile frnd match,, yanga vs JKT yanga walishinda goli 2 kwa kubebwa jkt wali shine 65%
    yanga vs A.lion, Lion wali posses 65% yanga vs cost union, Coast wali posses 70% sasa na bado mech za ki toto hizi wana mfukuza coach baada ya octber 3 watamfukuza MANJI.

    ReplyDelete