Search This Blog

Friday, March 15, 2013

KOCHA WA YANGA: NAHITAJI USHINDI KWENYE MECHI TANO ZIJAZO

KOCHA wa Yanga, Mdachi Ernest Brandts amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanashinda mechi tano ikiwemo ya kesho dhidi ya Ruvu Shooting na kutwaa ubingwa kabla ya ligi kumalizika.
Yanga inaongoza ligi na pointi 45 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 37, bingwa mtetezi, Simba ni ya tatu na pointi 34.
Mholanzi huyo alisema jana jijini Dar es Salaam;"Nafikiri tuna nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu."
Alifafanua kuwa endapo Yanga itashinda mechi tano kati ya saba zilizobaki itafikisha pointi 60 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
"Tuna mechi saba mkononi, lakini tunatakiwa kushinda tano kati ya hizo kutawazwa mabingwa wapya wa ligi."
"Lakini, kama wachezaji wangu watabweteka, tunaweza kukashindwa kupata kile ambacho tulitarajia."
"Kwa hiyo, bado nasema Azam na Simba  ni wapinzani wetu wakubwa na wana nafasi ya kupambana na sisi katika kuwania ubingwa." alisisitiza kocha huyo.

1 comment:

  1. kombe ni letu halina ubishi simba na azam wajipange labda mwakani by Peter Ng'olah bugando university Mwanza

    ReplyDelete