Search This Blog

Thursday, March 14, 2013

SIMBA HAKIELEWEKI: HUKU KEITA AKIDAIWA KUTOROKA - MAFTAH NA NGELEMA WAGONJWA

SIMBA inakabiliwa na tatizo la beki wa kushoto baada ya mabeki wake wote wa kikosi cha kwanza kuwa majeruhi.
Timu hiyo ina mabeki wa kushoto wawili Amir Maftah na Paul Ngalema ingawa Shomari Kapombe naye humudu kucheza nafasi hiyo.
Maftah anasumbuliwa na 'enka' wakati Ngalema anauguza goti ingawa mwenyewe amekiri kuwa hivi sasa yuko fiti na anasubiri ruhusa ya daktari wa timu kuanza mazoezi mepesi.
Kutokana na tatizo hilo kocha Patrick amelazimika kumchezesha kinda Miraji Adam nafasi hiyo.
Lakini licha ya kudaiwa Maftah ni mgonjwa tangu acheze mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Libolo nchini Angola kuna taarifa za ndani zinadai mchezaji huyo amesimamishwa huku ikidaiwa kuwa kocha Liewig amepanga kutowatumia baadhi ya wakongwe katika michezo iliyobaki kutokana na nidhamu zao kuwa mbovu.
Kapombe ambaye humudu kucheza nafasi hiyo ya beki wa kushoto hawezi kutumika katika nafasi hiyo hivi sasa kutokana na mkanganyiko uliopo Simba hivi sasa hasa katika beki wa kati baada ya Juma Nyoso kuwa na kadi nyekundu huku Komanbil Keita raia wa Mali akitoroka katika timu hiyo na kuzima simu hivyo Kapombe hana budi kucheza nafasi ya beki wa kati kwa sasa.
Ngalema alisema kuwa hivi sasa anaendelea vizuri na ataanza mazoezi muda si mrefu lakini kwanza anasubiri ruhusa ya daktari ingawa aligoma kuhusisha ugonjwa wake na mambo ya kishirikina.
"Mimi naumwa kawaida tu,ingawa nimekaa muda mrefu lakini si kama nimelogwa, ingawa hayo mambo ya kishirikina yapo kwenye soka la bongo lakini huu ugonjwa wangu ni wa kawaida tu na hauhusiani na mambo hayo"alisema Ngalema ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Ruvu Shooting.

4 comments:

  1. Naona Kaburu na Hans Pope wameamua kuondoa wachezaji wao na kuwaambia wazime simu(Komabili Keita na Sunzu).Hii inathibitisha kuwa hawa jamaa walikuwa wanakula pesa kupitia hawa wachezaji sasa wanaona aibu kuwaacha pale wachezaji wapate pesa yao kamili.Simba mwendo mdundo na sasa timu ndiyo itakuwa nzuri ile mbaya maana makinda wataonyesha juhudi binafsi ili wapewe namba moja kwa moja.Kaburu+Hans Pope msirudi tena Msimbazi hatuwataki.

    ReplyDelete
  2. Simba ilikuwepo,ipo na itakuwepo bila hao wa2 hakuna aliyejuu zaidi klabu kwahy 2wape nafac vijana na wata2onyesha maajab 2!

    ReplyDelete
  3. Nafikiri huu ni wakati mzuri sn kwa viongozi wakumpa kocha sapoti na kumwacha awe huru ktk maamuzi yake hasa yakuwapanga vijana na kuunda timu imara ya Simba,,,,naomba viongozii muwatoe wachezaji wote wakongwe ambao mnaona hawana nidhamu,wasio ji2ma,,na nafac zao muwape vijana sisi mashabiki 2ko tayari kusubiri hata kwa miaka miwili maana timu ye2 ya vijnaa itakujaa kuleta mapinduzi ktk soko la bongo,,,,mashabiki na wanachama wa simba 2wape sapoti,,na 2we wavumilivu,,,kwa vijanaaa

    ReplyDelete
  4. Vijana uwezo wanao ni kupewa nafasi na kuaminiwa wanaweza tatizo la mpira wakibongo makocha huwa wanapangiwa timu ndio maana ha2pig hatua kma wenzetu, timu inasajili maprofessional tena wanalipwa fedha nyingi lakini uwezo wao tunakuwa na mashaka nao kamati za usajili je zina sajili kuzingatia matakwa ya kocha au ili mradi 2 watu wanakula hela ama timu imesajili mchezaj toka nje tena kwa sifa alafu mwsho wa siku hanma kitu,viongoz mbadilike angalien wenzetu wanafanya nin na nyie mnafanya vitugani.

    ReplyDelete