Search This Blog

Friday, July 5, 2013

HIGUAIN KUFANYIWA VIPIMO LEO NA KUSAINI MKATABA WA MIAKA 3 NA ARSENAL - WENGER AKIVUNJA REKODI YA ADA YA USAJILI



ARSENAL jana usiku walivunja rekodi yao ya usajili baada ya kukubaliana na Madrid kulipa kiasi cha  £23million kwa ajili ya kumsaini Gonzalo Higuain.

Muargentina huyo atafanyiwa vipimo na Gunners leo na anategemewa kusaini mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya100,000 kwa wiki.

Higuain, 25, amepewa ruhusa na Madrid kusafiri kwenda London baada ya mazungumzo marefu yaliyodumu kwa wiki kadhaa.

Dili hili ambalo limethibitishwa na baba yake Higuain linakuja kuleta nafuu kwa mashabiki wa Arsenal waliokuwa wakililia kocha wao asajili wachezaji wa daraja la dunia, ili kuweza kukata kiu ya zaidi ya miaka nane ya kutwaa kombe.

Santiago Cazorla ndio alikuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Arsenal - akiwa amesajiliwa kwa zaidi ya paundi millioni 16 akitokea Malaga.


Golikipa Julio Ceasar ndio anatajwa kumfuatia Higuain kwenda Emirates akitokea QPR ambao wameshuka daraja.

7 comments:

  1. habari njema sana hii kwa wanaArsenal ulimwenguni kote!!

    ReplyDelete
  2. WE JUS STILL WAIT AND SEE HOW THE NEW SEASON WILL START AND ENDING,,,PAUL SULEIMAN..

    ReplyDelete
  3. Babu Aongeze striker Wa Ukweli tena, Huyu Jamaa Amekaa Benchi Sana Mbele Ya benzema na ronaldo, ingawa Benzema hayuko vizuri kiivyo, babu avunje Kibubu alete majembe ya ukweli haya huwa yanauzwa kuanzia 30m nakuendelea sio watu ambao hawatakiwa na klabu zao

    ReplyDelete
  4. good news!! bado Caser, rooney, jovetiv and fellain, uza arshavin, benditna,chamack,denlson, manone,seshny n.k

    ReplyDelete
  5. amuongeze fellaini na cesar julio, mwaka kesho tunachukua trebble kama ya bayern munich

    ReplyDelete
  6. good news to all arsnl fans!hope other signings to come to strengthen our squad...

    ReplyDelete
  7. unaonaje ukiwa unapost information za kweli zilizokua confirmed na club husika na sio rumours toka kwa journalists twitter or goal.com,suala la higuain ni danadana mwez sasa,mpaka sasa hajafanyiwa medical tests na hakuna club iliotangaza makubaliano baina yao.mtazamo tu.

    ReplyDelete