Search This Blog

Saturday, July 6, 2013

PAULINHO ATAMBULISHWA RASMI TOTTENHAM HOTSPUR - EKOTTO ADAI HAMJUI KABISA

 Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Paulinho leo ametambulishwa na Tottenham baada ya kukimilisha uhamisho wa paundi millioni 17 Corinthians ya Brazil. Lakini wakati mchezaji huyo akitambulishwa mchezaji mwenzie wa timu hiyo beki wa kimataifa wa Cameroon
Assou-Ekotto ameiambia Goal.com: ' Simfahamu hata alivyo. Simjui, mie sifuatilii habari za namna hiyo. Mfano mzuri ni miaka mitatu iliyopita, Rafael van der Vaart alikuwa ndio amekuja mazoezini mara ya kwanza, nilimsalimia lakini sikuwa najua kama yeye ndio Rafael van der Vaart."


6 comments:

  1. vEkoto mjeuri tu ina maana hajaangalia nusu fainal ya brazil na uruguay?au pia hata fainal ya kombe la mabara?hajafanya uungwana bora angesema anamfahamu ila sio sana.ubinafsi sio kitu kizur mchezaj na mpenda soka hawezi shindwa tazama kombe la mabara hata kwa baadh ya mech hususa kuanzia robo fainal.inawezekana hamjui hata rais wake wa cameron au kama cameron imefungiwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. USIMFIKIRIE VIBAYA EKOTTO ,HUYU JAMAA ANASEMA KUWA SOKA ANACHEZA TU KWA KUWA NDIO INAMUINGIZIA MSHIKO ILA YEYE SIO MPENZI NAYO ,HVYO HAFUATILII HATA HABARI ZAKF!

      Delete
  2. Inawezekana mkasema jeur ila mim cna uhakika kwa hilo, nakumbuka ekotto ashawah kukir kuwa yeye habar za mpira znaishia uwanjan akitoka hafatlii tena, c mpenz wa kuangalia mpra.. n nje ya uwanja hafatilii kabsaaa.... kunauwezekano ikwa kwel.. wangap kabla ya michuano hyo walikuwa wanamjua paulinho?? Msihukumu watu
    By
    Makaveli Jr.

    ReplyDelete
  3. Ekoto ni mwanamuziki mpira analazimisha tu sbb hakuwa na promo ulaya,ndiyo maana hata mpira kwenye TV huwa haangalii.Nadhani ingekuwa nzuri sanaa kama angeambiwa kuwa huyu amekuja kuchukua namba yako hapo nadhan angefanya juhudi za kutafuta mikanda ya huyo jamaa ili amjue yuko vipi haswa.

    ReplyDelete
  4. atamjua siku atakapokuwa anashangiliwa na mashabiki wa spurs ndani ya whitehart lane. I hope mashabiki watampenda na kumshangilia kumzidi yeye (ekotto). Hiyo sio tabia nzuri, ni bora angekaa kimya.

    ReplyDelete
  5. ''Simfahamu hata
    alivyo. Simjui, mie sifuatilii habari za namna hiyo''. Ingawa goal.com si mtandao wa kuaminika sana lakini kama ni kweli ni kauli ya kushangaza. Inaonyesha ekotto yuko spurs kwa ajili ya pesa tu na afuatilii mipango ya klabu. Wachezaji wengi wanataka kujua timu zao zina malengo gani ya mbele ambayo pia inahusisha usajili. Ina maana ekotto hajui anataka nini. Kama anasema afuatilii habari za namna hiyo sasa anafuatilia nini? Pesa kama imeingia kwenye kila wiki

    ReplyDelete