Search This Blog

Sunday, July 7, 2013

YAFICHUKA: MAKOCHA WA NIGERIA STEPHEN KESHI NA DANIEL AMOKACHI HAWAJALIPWA MIEZI MITANO


Kocha wa Nigeria Stephen Keshi hajalipwa mshahara wake tangu alipoiongoza Super Eagles kushinda ubingwa wa watatu wa mataifa huru ya Afrika miezi mitano iliyopita.
Lakini kocha huyo ambaye ni nahodha wa zamani wa Nigeria hajatoa malalamiko rasmi kuhusu suala hilo. 
Na shirikisho la soka la Nigeria limeiambia BBC kwamba suala hilo linashughulikiwa. 
"Kati ya upande wa shirikisho na kocha mwenyewe hakuna tatizo," alisema katibu mkuu wa NFF Musa Amadu.
Continue reading the main story
Obligations to the coaching crew are always settled, and we have the understanding of the coaching crew in this regard
Musa AmaduNFF general secretary
"Tumekuwa tukifanya kazi na Stephen Keshi tangu November 2011 na anajua kwamba kuna matatizo ya kifedha ndani ya shirikisho.
"Tunajaribu kwa kila namna kulipa madeni yetu, tuna mahusiano mazuri ya kikazi.
"Nafahamu kwamba kocha hatopeleka suala hili mbili sheria," aliongeza.
NFF, ambayo ina matatizo ya kifedha, pia inadaiwa na kocha msaidizi wa Daniel Amokachi mkufunzi wa magolikipa Ike Shorunmu.
Shirikisho hilo la soka ambalo linapokea ruzuku kutoka kwa wizara ya michezo, imekubali kwamba inadaiwa na makocha na imewaomba kuendelea kuwa wavumilivu. 
Hii sio mara ya kwanza kwa makocha wa wanageria kutokulipwa. 
Mwezi December mwaka jana, NFF ilithibitisha kwamba inadaiwa mshahara wa miezi miwili - wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa mataifa huru ya Afrika 2013.

No comments:

Post a Comment