Search This Blog

Sunday, July 7, 2013

DAVID MOYES NA UTEUZI WA WAKONGWE RYAN GIGGS NA NEVILLE UNATOA PICHA YA MANCHESTER UNITED YA BAADAE



David Moyes ameanza kazi rasmi ya kuifundisha Manchester United manager pale Old Trafford siku kadhaa zilizopita huku akitangaza wale wataomsaidia kazi katika kui-mange klabu hiyo kubwa duniani.
Ikiwa mshabiki wa Manchester United watakuwa na wasiwasi na ubora walionao wale wasaidizi Moyes amekuja nao kutoka Everton, then uteuzi wa watu ambao walikuwa wakiaminiwa mno katika kizazi cha dhahabu cha Sir Alex Ferguson kidogo unaleta nafuu ya wasiwasi. 

Jukumu la kwanza Moyes tangu alipomrithi Ferguson ilikuwa kuwaleta watu ambao ana mazoea ya kazi kutoka kwenye miaka 11 aliyofanya nao kazi Everton. Wamekuwa na uzoefu mkubwa na premier league kama yeye mwenyewe - lakini hawatoi uhakika wa kubeba taji mara kwa mara ambao unahitajika ndani ya United.
Hapa ndipo alipoteuliwa mchezaji mkongwe zaidi kwenye kikosi cha United na mwenye mafanikio, anayeijua timu kuliko - Ryan Giggs. Akapewa jukumu la kuwa kocha mchezaji, na pia akaongezwa Phil Neville - mtu mwingine ambaye anatoka kizazi cha dhahabu cha Sir Alex Ferguson. 
Steve Round alitumia miaka mitano kufanya kazi kama msaidizi wa Moyes pale Everton na sasa atakuwa na jukumu hilo hilo pale Old Trafford. Pia amewahi kufanya na mtu mwingine anayeijua vizuri United - Steve McClaren wakati akiwa kocha wa England na klabu ya Middlesbrough. Round anaheshimika sana kwenye soka, lakini sio kwenye daraja la dunia. 
 Scot Jimmy Lumsden inawezekana ndio mtu ambaye anaaminika zaidi na Moyes, amekuwa akifanya kazi na Moyes tangu wakiwa Preston na mpaka Everton, wakati Chris Woods amekuwa kocha magolikipa pale Goodison Park tangu mwaka 1998.

Kazi ya Woods, itakuwa ngumu zaidi , katika kukiboresha kipaji cha golikipa kinda wa kihispania David de Gea kama ilvyokuwa kwa kocha aliyepita Eric Steele aliyemjenga vizuri kipa huyo msimu uliopita na kusababisha kuingia kwenye timu ya mwaka ya PFA.
Uteuzi wa jopo hili la makocha unaweza usiwe na ushawishi mkubwa miongoni mwa mashabiki wa United ambao bado wanampima Moyes, lakini hii ni hatua muhimu kwa Moyes akiwa ndio anaanza kazi ya kuiimarisha klabu hiyo yenye mafanikio zaidi nchini Uingereza. 

Kwa namna ambavyo Moyes amefurahia kuwaweka watu anaowajua na kuwaamini kwenye kumsaidia kazi yake, lakini pia anaelewa kwamba anahitaji kuonyesha kwamba wana uwezo wa kuielewa United na utamaduni wake - na hapa ndipo anawateua watu wanaijua vizuri namna United inavyofanya kazi.
Giggs, atakuwa na miaka 40 mwezi November na ndio mchezaji wa kiingereza mwenye mafanikio zaidi akiwa na makombe 13 ya premier league na mawili ya Champions league, japokuwa bado anacheza hasa baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja mwezi March, lakini hawezi kushindana na muda zaidi hilo analijua ndio maana ameanza kujiandaa kuchukua jukumu lingine ndani ya klabu - na baada ya kuondoka kwa Steele, basi kama kuna mtu anafaa kuirithi nafasi yake ndani ya klabu hiyo - basi ni Giggs. Anategemea kupata leseni ya ukocha kutoka UEFA baadae mwakani na tayari ameshaonekana kuwa ndio manager wa Manchester United atakayefuatia huko baadae
.

Hakuna mchezaji wa kikosi cha sasa ambaye anaheshimiwa na wachezaji kama Giggs na ndio mtu atakayekuwa daraja baina ya chumba cha kubadilishia nguo pale Old Trafford na ofisi ya maneja. 
Neville, 36, alijitengenezea sifa nzuri kwa mwenyekiti wa Everton  Bill Kenwright alipofanyiwa usaili wa kushika nafasi ya uongozi pale Goodison wakati Moyes alipoamua kuondoka. Angeweza kuchagua kufanya kazi na kocha mpya wa Toffees Roberto Martinez lakini mapenzi ya klabu yake ya utotoni yakamvutia kurudi Old Trafford - mahala ambapo alishinda mataji sita akiwa chini ya kizazi cha dhahabu cha Ferguson. 
Tayari alishatambuliwa na FA kama kocha - baada ya kuteuliwa kwenye jopo la makocha waliiongoza England Under-21 team katika Euro huko Israel. Neville ni mtu muhimu kwenye Manchester kwa sasa akiwa anaijua kiundani klabu na pia anamfahamu Moyes na utendaji wa kazi yake kwa kuwa amekuwa nae kwa miaka nane pale Everton. 
Na kwa klabu ambayo ilimteua kocha Moyes kwa kuangalia umadhubuti, uamuzi ambao ulifanywa kwa nguvu ya ushawishi wa Ferguson, wakimuacha kocha ambaye ni mzoefu zaidi na mwenye ushawishi lakini ambaye hatoi uhakika wa kudumu na timu kwa muda mrefu - Jose Mourinho, United ni taasisi inayojipanga namna ya kuishi kwa miaka mingi mbeleni. 
Ndio maana wachambuzi wa soka wanasema kwamba uteuzi wa Giggs na Neville huku Paul Scholes akiwa tayari ameanza mafunzo ya ukocha kama ilivyo kwa Nicky Butt - Manchester United inawaandaa vijana hwa wanaoijua vizuri klabu hii kuja kumrithi Moyes huko mbeleni. 
Kila kocha duniani anapenda kufanya kazi na watu ambao anawafahamu. Moyes yeye amefanya hivyo pia kwa kuwaleta watu ambao ametoka nao Everton. Kwake hii ni kombinesheni nzuri.
Giggs ni daraja baina yake na wachezaji hasa ikizingatiwa yeye ni mpya klabuni, wakati Neville ambaye anaijua vizuri aina ya utendaji wake wa kazi na pia wa klabu ya Manchester United, pia ni gwiji wa klabu.




1 comment: