Search This Blog

Saturday, March 24, 2012

MESSI NAE AVUNJA REKODI YA RONALDO DE LIMA BARCELONA

Lionel Messi nae ameendelea na uvunjifu wa rekodi katika klabu yake ya Barcelona, baada ya hivi leo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa La Liga, kufuatia kutia kambani katika mechi dhidi ya Real Mollorca.

Messi amevunja rekodi ya Ronaldo De Lima aliyefunga magoli 34 katika msimu wa 1996-97, kwa sababu goli lake la leo hii linamaanisha amefikisha idadi ya magoli 35 ya la liga pekee msimu huu.

Messi sasa anaikimbiza rekodi ya Cristiano Ronaldo aliyoiweka msimu uliopita kwa kufunga magoli 40 ndani ya msimu mmoja na kumfanya awe mfungaji bora wa muda wote wa ligi katika kipindi cha msimu.

1 comment:

  1. Kumbe amevunja rekodi ya Barcelona tu? Lakini Cristiano Ronaldo bado anaendelea kuvunja rekodi japo vyombo vya habari vinafocus kwa Messi tu

    ReplyDelete