Search This Blog

Friday, March 23, 2012

EXCLUSIVE: SIMBA YAMSAJILI MWANAJESHI NA MCHEZAJI ANAYELIPWA FEDHA NYINGI KULIKO WOTE UGANDA NA KENYA.


Klabu ya Simba imemsajili kiungo Musa Mudde kutoka klabu ya Sofa paka ya Kenya.
Musa Mudde ni raia wa Uganda na ndio mchezaji aliyekuwa akishikilia rekodi ya kuwa mwanasoka anayelipwa mkwanja mrefu kuliko wote katika ligi kuu ya Kenya na Uganda.
Musa Mudde ameingia mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba, na ataanza kuvaa jezi nyeupe na nyekundu kuanzia msimu ujao.
 Kiungo huyo ambaye  ana miaka 22 alianza kuichezea klabu ya jeshi la UPDF - Simba FC ya nchini kwa o Uganda, kabla ya kuhamia nchini Kenya katika uhamisho ulioleta mtafaruku mkubwa.
Akiwa kama mwajiriwa wa jeshi alikuwa haruhusiwi kwenda kucheza soka la kulipwa sehemu nyingine nje ya jeshi, ilibidi mpaka akaombe ruhusa kwa mkuu wa majeshi wa Uganda na amiri jeshi mkuu wan chi Raisi Yoweri Museven ndipo alipokubaliwa kwenda kucheza nchini Kenya, ambapo ndipo alipokuwa mchezaji anayekusanya mkwanja mrefu kuliko mchezaji yoyote ndani ya Uganda ama Kenya, akilipwa kiasi cha shilingi za Kenya 83,000 kwa mwezi.
Mudde sasa anaingia Simba akiwa kama replacement ya kiungo Jerry Santo

1 comment:

  1. Jamaa bonge la Midfilder, nimejaribu kuangalia clip yake online akiwa na Uganda cranes pamoja na Sofapaka anaonekana ni mchezaji mzuri kwa kweli na wachezaji wa kiganda wanaonekana kuimudu vema ligi ya bongo anaweza leta changamoto kwenye timu ya Simba.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete