Roman Abramovich yupo tayari kumpa super-coach Pep Guardiola mkataba wa miaka minne wenye thamani ya £40million baada ya kodi ili awe kocha wa Chelsea.
Billionea huyo wa kirusi na mmiliki wa klabu hiyo ameonakana kukataa kukata tamaa katika harakati ya kumsaini kocha huyo.
Hivyo kwa mkataba huo utamfanya Guardiola kama kocha anayelipwa fedha nyingi kuliko wote katika soka duniani, akimlipa Guardiola £10million kwa mwaka kwa cash, kwa mujibu wa mtu wa ndani kutoka Chelsea.
Guardiola na dili lake pale Nou Camp linaishia mwishoni mwa msimu na Abramovich ameapa kutoacha kumfuatilia kocha huyu, huku Pep mwenyewe akiacha hatma yake ikiwa bado haijafahamika mpaka sasa.
Kwa sasa Pep analipwa £8milion kwa mwaka pale Barca lakini Roman anataka kumuongezea shavu kwa £2million zaidi.
No comments:
Post a Comment