Search This Blog

Friday, March 23, 2012

ZENGWE LINGINE LAIBUKA MKOANI LINDI !



Habari yako kaka Shaffih! kwa muda mrefu tulikua tunakosa pa kusemea yanayotusibu hasa sisi tuliopo mbali na Dar Es salaa,
nitumie nafasi hii kuwapongezi CLOUDS FM na kipindi chenu cha SPOTI EXTRA pamoja na BLOG yako kaka shaffih, sasa sikia haya madudu kwenye mpira wetu huku mkoani LINDI,


Sisi beach boy’s ya Lindi mjini tunamalalamiko kuhusu jinsi uendeshajiwa ligi ya mkoa kunaubabaishaji mkubwa uliofanyika, sisi tumemaliza ligi tukiwa na point 6 na mechi zetu mbili hazikuchezwa bila sababu za msingi mechi ya kwanza dhidi ya Bridgestone tulipata ushindi wa bao 1-0 mechi ya pili tulipata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Lumbesa Kilwa .


Sasa mechi ya tatu dhidi ya Lindi S.C ndipo zengwe ilipoanza kwani mvua ilizuia mechi na mechi iliahilisha kutokana na kanuni za ligi zinavyosema mchezo wowote unaohailisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa binadamu basi mchezo utapangwa tarehe nyingine au utachezwa siku ya pili endapo ratiba itaruhusu .


Kutokana ratiba ilikuwa inaendelea tulijua fika mchezo ungekua kipolo lakini kwa mshangao wa wengi tuliletewa barua saa 7.30 siku ya pili mchana tukitakiwa tupeleke timu uwanjani kwa ajili ya mchezo sisi tulifungua kitabu cha kanuni ndipo tulipokikuta kifungu cha 9 (d) kinataka sisi kucheza kwani siku hiyo kulikua na mchezo kati ya Bridgestone dhidi ya Mnazimmoja ya Kilwa tuliwaandikia kuwaeleza ya kuwa hatutapeleka timu kisheria kwa ajabu wenzetu wapewa ushindi kinyume na kanuni zinanyoeleza ajabu zaidi klabu hatujajibiwa dai letu siku 1 kabla ya mchezo wetu wa mwisho kati yetu na Mnazimmoja ya Kilwa tuliletewa barua ya kuadhibiwa kutokana kutoleta timu uwanjani.


Naambatanisha pamoja na barua hiyo ya adhabu ambazo hazilingani na kosa sisi tulipinga adhabu hizo kwa maandishi na siku ya mchezo maandalizi ya kabla ya mchezo yalifanyika tulifika uwanjani pamoja na wapinzani wetu na waamuzi cha ajabu uongozi wote waTFF haukuwepo waamuzi wakaeleza hawana mamlaka ya kuchezesha bila idhini ya viongozi wa TFF ambao hawakuwepo uwanjani


Sisi kwa kuthamini umuhimu wapenzi wa mchezo huo waliofika uwanjani tulikubaliana na wenzetu tulicheza mechi ya kirafiki


Ligi imekwisha tuna point 6 mechi mbili mkononi timu zote zilizobaki zina point 3 kasoro Lindi S.C na hatujapata barua elekezi ila tunasikia eti timu yenye point 3 ndio itakayopata nafasi sisi tumeamua kuweka wazi ubabaishaji huu kwani Lindi huku umekithiri tunaomba wanaosimamia soka letu walitambue na wafuatilie sakata hili

No comments:

Post a Comment