Search This Blog

Saturday, June 30, 2012

JERRY TEGETE APIGA BAO MBILI: YANGA IKIWAFUNGA WAGANDA EXPRESS 2-1


Mabingwa watetezi wa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME) timu ya Young Africans Sports Club imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya Mabingwa wa ligi kuu ya Uganda timu ya Express FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans iiliyotimia fursa hiyo kuwatambulisha wachezaji wapya iliyowasajili katika msimu mpya wa ligi kuu ya VPL na mashindano ya kimataifa Kagame,lianza mchezo kwa kasi na katika dakika ya 1 ya mchezo, mshambuliaji aliyesajiliwa kutokea Moro United Saimon Msuva alipiga shuti kali liliotoka sentimeta chache ya lango la Express.
Dakika ya 3 ya mchezo mshambuliaji Jeryson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza, mara baada ya kumalizia krosi safi iliyopigwa na mshambuliaji mpya mwenye misuli kutoka Mtibwa Sugar Said Bahanunzi.
Huku ikicheza soka safi nala kuvutia, Young Africans iliendelea kulishambulia lango la Express muda wote wa mchezo huku eneo la kiungo likimilikiwa vizuri na chipukizi Frank Domayo aliyesajiliwa kutoka JKT Ruvu, Chuji, Nizar Khalfan.
Jeyson Tegete aliendelea kuwa mwiba kwa waganda hao, kwani katika ya 19 ya mchezo, Tegete aliipatia tena Young Africans bao la pili akimalizia krosi safi ya Said Bahanunzi aliyeonekana kuisumbua gome ya Express.
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, Young Africans ilikuwa mbele kwa mabao 2- 0.
Kipindi cha pilik kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo iliwapumzisha Kelvin Yondan, Oscar Joshua, Jeryson Tegete, Nizar Khalfan, Said Bahanunzi na Saimon Msuva na nafsai zao kuchukuliwa na Ladisalus Mbogo, Stephano Mwasika, Hamis Kiiza, Omega Seme, Idrisa Rashid na Shamte Ally.
Mabadiliko hayo yaliipa uhai timu ya Express kwani ilianza kulishambulia lango la Young Africans na katika dakika ya 73 ilipata bao la kufutia machozi, baada ya kupiga faulo iliyowachanganya walinzi wa Young Africans na kukuta wakijifunga.
Mpaka dakika 90 za mwamuzi Oden Mbaga zinamalizika Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi wa wageni Express kutoka Uganda.
Young Africans iliwakilishwa na:
1.Barthez, 2.Juma Abdul, 3.Oscar/Mwasika, 4.Cannavaro, 5.Yondan/Mbogo, 6.Chuji, 7.Nizar/Shamte, 8.Frank Domayo, 9.Said Bahanunzi/Omega, 10.Tegete/Kiiza, 11.Msuva/Idrisa

No comments:

Post a Comment