Search This Blog

Friday, June 29, 2012

HIVI NDIVYO MAGAZETI YA UJERUMANI YALIVYOWAKEJELI WAITALIA JANA MCHANA - KABLA YA BALOTELLI HAWAJAFUNGA MIDOMO


Kwa kuangalia rekodi yao nzuri kwenye Euro 2012, watu wengi waliamini kwamba Ujerumani wangekuwa na kazi rahisi ya kuwaondoa waitaliano kwenye mchezo wa nusu fainali wa Euro.

Mario Balotelli akawafanya watu wengi jana kukosea kwenye utabiri wao na sasa Wajerumani na mashabiki wao wanajiuliza nini hasa kilichotokea.
(Shukrani kwa wachezaji wa Bayern kwenye kikosi angalau wanaweza kuwaonyesha wenzao namna ya kuugulia maumivu ya kupoteza ubngwa ambao takribani nusu ya washabiki wa mpira duniani tulikuwa tunaamini wangeweza kuuchukua safari hii.)

Kwa upande mwingine gazeti la kila siku la Bild la Ujerumani nalo liliingia mkenge kwa kuiamini sana timu yao taifa dhidi ya Italy - walichapisha picha kubwa kwenye website yao ikionyesha ndege kubwa ya Italy ikiwa imewabeba wachezaji wa Azzuri tena wakiwa wamepangwa kwa formation kabisa - wakielekea nyumbani baada ya kutolewa kwenye mashindano na Ujerumani - na wakaandika maneno ya "Tunawatakia safari njema ya kurudi nyumbani."

Kwa sababu wazijuazo wenyewe - ile picha ya waitaliano wakiwa mfumo wa kiuchezaji wakirudi nyumbani kwenye ndege imetolewa kwenye mtandao wa Bild.

Bild halikuwa gazeti pekee la kijeumani lilopata aibu kwa matokeo ya jana usiku. Hamburger Morgen Post - wenyewe walichapisha picha kubwa kwenye ukurasa wao mbele wa gazeti - wakiweka Pizza ya pepperoni ya kiitalia huku ndani yake zikionekana picha za wachezaji wa Italia.

Chini ya picha ile wakaandika maneno ya kejeli kwa Waitaliano yaliyosomeka, "Mwisho wa Pizza" kama kichwa cha habari kikuu huku vkichwa cha habari kidogo kikiandika - "Sababu 11 kwanini tutawaondoa Waitalia mashindanoni leo usiku"

Lakini kwa bahati mbaya sana kwa gazeti hili la kijerumani kitu pekee walichokuala jana suiku ni maneno yao - shukrani kwa Balotelli.

1 comment:

  1. wakuu heshima yenu!! awali ya yote ni wape poleni kwan mlikuwa miongozi mwa watabili feki ya kwamba ujerumani angemtoa itally.
    awali niliona kabisa italy ndo bingwa wa michuano hii na ndo itakavyo kuwa kwasababu spain nae atafungwa goli nyingi kuanzia tatu.dunia lazima itambue kuwa italy ilibolonga kombe la dunia inachofanya sasahivi ni kujivua gamba na kuhiakikishia dunia kuwa wanaweza

    ReplyDelete