Search This Blog

Friday, June 29, 2012

OKWI KWENDA ITALIA TAREHE 4 JULAI KUFANYA MAZUNGUMZO YA KUJIUNGA NA PARMA

Hayawi hayawi sasa yanaeleka kutimia.

Kumbuka siku chache zilizopita nilitoa taarifa juu ya mshambuliaji Emmanuel Okwi kuwa lulu kwenye soko la usajili, akitakiwa na vilabu vikubwa vya South Africa Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns huku kukiwa na klabu inayoshirki ligi kuu ya Italia Serie A nayo ikimuwania.

Sasa zilizothibitishwa na uongozi wa Simba ni kwamba mnamo tarehe nne mwezi ujao, Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda na mabingwa wa Tanzania bara Simba anatarajiwa kukwea pipa kuelekea nchini Italia kufanya mazungumzo ya klabu ya Parma kwa ajili kuweza kujiunga nayo kwenye msimu ujao.

Ikiwa Okwi atafanikiwa kufikia makubaliano na Parma na kuweza kujiunga nayo Simba inategemea kuvuna kiasi cha fedha kisichopungua billioni mbili mpaka nne kama ada ya uhamisho wa Okwi.

Kila kheri la Okwi.

6 comments:

  1. Simba ni njia panda ya ulaya. Ukitaka kwenda ughaibuni basi chezea Simba

    ReplyDelete
  2. Kaka unapenda sana kudanganya watu, Okwi hawezi kununuliwa zaidi ya billion mbili au nne...Parma hawajawahi kufanya uhamisho wa mchezaji yeyote zaidi ya Euro 600,000 ingia kwenye website yao...thanks.
    Mdau
    Italy

    ReplyDelete
  3. Bro! Acha kujidhalilisha kwa kutoa ushahidi wa VIONGOZI wa simba (Hasa RAGE). Viongozi wasiokuwa na AIBU wala HAYA, watu wanatufanya cc wanachama na wa Simba kwa ahadi nyingi amabazo zimekuwa nia aibu hata kuzitaja. Wewe ni mwandishi wa habari fanya uchunguzi wako binafsi ili u explore information, wale Parma wana WEBSITE yao na kuna kipengele cha afisa habari wasiliana nae upate uhakikisho wa habari yako vinginevyo kila siku utakuwa ni mtu wa COPY AND PAST taarifa za wenzio jaribu na wewe siku moja uwe chanzo cha kuaminika. Ni ushauri tu ukipenda chukua hutaki acha.

    ReplyDelete
  4. namtakia kila la heri cause mafanikio yake ndiyo mafanikio ya nchi yake,club yake na wachezaji wenzake.keep it up man

    ReplyDelete
  5. kiukweli jamaa mkali astahili kkucheza east africa kwa kiwango chake alichoonyesha tangu ajiunge na simba sc kila la heri. its me kwanja jr from ilala fc boom

    ReplyDelete
  6. Czan kama kunaukweli Okwi kwenda Parma

    ReplyDelete