Search This Blog

Friday, February 3, 2012

BREAKING NEWS: FA WAKUTANA LEO KUZUNGUMZA JUU YA UNAHODHA WA JOHN TERRY KATIKA KIKOSI CHA ENGLAND.


Saa chache baada ya moja ya wachezaji wa zamani Jason Roberts kusema John Terry ni sumu katika kikosi cha England, viongozi wa chama cha soka cha England FA wanaweza wakaamua kumvua  kitambaa cha unahodha Terry leo hii Ijumaa.
Mwenyekiti wa FA, David Bernstein amewasiliana na wanachama  12 wa bodi ya juu ya maamuzi jana Alhamisi kusikiliza mawazo yao juu ya suala la Terry.
Inavyoonekana wengi wa wanachama wa bodi hiyo hawadhani kama ni jambo sahihi kwa Terry kuwaongoza waingereza katika EURO 2012 huku akiwa na mashtaka ya matusi ya kibaguzi wa rangi, na wanaona FA kwa haraka inabidi ifanya maamuzi haraka kabla ya mkutano wa February 23 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment