Search This Blog

Friday, February 3, 2012

GIGGS: TUKIVUKA MWEZI HUU SALAMA TUNACHUKUA TENA UBINGWA.


Ryan Giggs anaamini kombe litabaki Old Trafford ikiwa Manchester United wataupita vizuri huu mwezi.
United watawatembelea Chelsea Jumapili hii, baadae watakutana na Liverpool na Tottenham, huku wakifunga mwezi huu kwa mechi ya ugenini dhidi ya Norwich.
Vijana wa Sir Alex Ferguson waliwakamata City kileleni wiki hii baada ya kuwafunga Stoke.
Na veteran huyu mwenye makombe 12 ya premier leaguae, Giggs anajua thamani ya kombe watakaloshinda kwa kuwashinda mahasimu wao wakubwa.
Alisema, “Tumeshaanza kurudi kwenye form yetu na kama tutapata matokeo mazuri katika michezo hii, confidence itakuwa juu sana.
“Tunafahamu ni mbio ngumu, lakini hiyo ndio michezo ambayo kila mtu anataka kucheza. Tunajua hii ni michezo muhimu sana, na tunafahamu kama tutashinda mechi hizi, then tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuutetea ubingwa wetu.
“Tunajua kilicho mbele yetu na nini tunapaswa kufanya.”

No comments:

Post a Comment