Search This Blog

Friday, February 3, 2012

FIFA: TUNAHITAJI RIPOTI NZIMA YA TUKIO LA VURUGU MISRI


Shirikisho la soka duniani FIFA limeomba kupatiwa ripoti nzima ya tukio la vurugu lilitokea nchini Misri ambalo limeacha watu zaidi ya 70 kufariki dunia.
FIFA imetoa amri kwa mamalaka ya soka  nchini Misri kuelezea kila kitu nini kilitokea katika mechi kati ya AL-Ahly na AL Masry jana jumatano.
Raisi wa FIFA Sep Blatter amemwandikia raisi wa FA ya Misri Samir Zaher.
“Leo ni siku nyeusi katika soka na lazima tuchukue hatua kuhakikisha tukio kama lile halijirudii tena. Soka ni mchezo wa nguvu zinazotumika kwa mazuri na lazima tusiruhusu zitumike vibaya kwa wale wenye mambo mabaya. Nasubiri habari zaidi kuhusu tukio lile.”
Maofisa wakubwa katika chama cha soka cha mji wa Port, ambapo ndipo tukio hilo lilipotokea , na viongozi wengine wa FA tayari wameshafukuzwa kazi.
Pia gavana wa mji wa Port ameshajiuzulu huku maofisa wawili wa juu wa usalama tayari wakiwa washasimamishwa na wapo chini ya ulinzi.
Siku 3 za maombelezo zimetangazwa na serikali. Pia kutakuwa na muda wa kukaa kimya katika mechi za robo fainali za African cup of Nations.

No comments:

Post a Comment