Search This Blog

Saturday, February 4, 2012

Na Mwandishi Wetu

Abdalah Mohamed 'Prins Naseem KUTETEA UBINGWA WAKE NA Salehe Mkalekwa
.Februari 24
BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST)
Abdalah Mohamed 'Prins Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake
wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa.
Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 57
na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi
'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New
Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.
Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho
hilo kuendelea kuwainua mabondia chipkizi ambao hawajawa na majina
makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.


"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio
maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni
kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.
Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa
kati ya Shaaban Zungu na Hasan Salehe watakaopigana uzito wa kg 55,
Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey
Pacho atakayetwangana na Seleman Shaaban na Abdalah Yusuph
atakayepigana na Omari Kijepa.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye
mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth,
Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali
ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila
‘Super ‘D’.

“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika
pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo
wa ngumi,” alisema Super ‘D’



Kocha wa mchezo wa ngumi Saba Joseph (kulia) akimwelekeza bondia Saleh
Mkalekwa jinsi ya kutupa masumbwi katika kambi yake iliyopo Mbagala
Mkalekwa anajihandaa na mpambano wa ubingwa wa PST na Abdalah Mohamed
'Prins Naseem' Februari 24.(Picha na
www.superdboxingcoach.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment