Search This Blog

Saturday, February 4, 2012

FERGUSON: NI MUDA WA KUWAFUNGA CHELSEA UWANJANI KWAO SASA


Alex Ferguson amekiri sasa ni muda sahihi kwa Manchester United kumaliza rekodi yao mbaya katika uwanja wa Stamford Bridge.

Fergie hajawahi kuifunga Chelsea ugenini katika Premier league tangu 2004 na amepata pointi 3 kutoka katika 27 @Stamford Bridge.
Boss huyu wa United alisema: “Tumefanya vizuri sana ugenini msimu huu na tunahitaji kuendelea kufanya vizuri hata sasa.

“Tuna michezo muhimu ya ugenini muhimu mno katika mbio hizi za ubingwa – Chelsea, Tottenham na City.
“Mechi dhidi ya Chelsea katika miaka ya karibuni zimekuwa ngumu sana na tuna bahati mbaya sana pale Stamford Bridge. Wachezaji wangu wanajua nini cha kufanya.”

United wapo sawa kwa pointi na City katika msimamo wa ligi kuu ya England.
Wamepunguza pengo la pointi japokuwa na wakati mgumu walionao kutokana na majeruhi kuwa wengi katika kiksi chao, na sasa inaonekana watarudi katika form yao ya mwanzoni mwa msimu kwa wachezaji wengi wanaanza kurejea.

Fergie ana matumaini mtoto wa maajabu Tom Cleverley, 22, yupo tayari kurudi dimbani tangu alipopata majeruhi katika mechi dhidi ya Bolton mwezi September mwaka jana.
Ferguson : “Alikuwa hatari mwanzoni mwa msimu na itakuwa kama tumesajili mchezaji mpya kwa kuwa na Tom katika kikosi chetu. Nafikiri ni Cleverley ni mchezaji muhimu na anatafanya mabadiliko makubwa katika mbio za ubingwa.”

No comments:

Post a Comment