Search This Blog

Wednesday, November 27, 2013

"MWENYE KIWANGO KIKUBWA NDIO NITAMPANGA." KOCHA WA YANGA AWAAMBIA KASEJA, DIDA NA BARTHEZ

KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amewaambia makipa wake Juma Kaseja, Ali Mustapha 'Barthez' na Deogratius Munishi 'Dida' kuwa kipa mwenye kiwango kikubwa ndiye atampa nafasi kwenye kikosi chake hicho.
Hiyo ni siku moja tangu kocha huyo aanze mazoezi na timu yake iliyoanza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Brandts alisema hatampanga mchezaji kutokana na ukubwa badala yake kiwango chake uwanjani.
Alisema, kwenye kikosi chake hadi hivi sasa hakuna kipa namba moja, yeye anaangalia uwezo na kujituma kwa mchezaji katika mazoezi yake.
"Nitampanga golini kipa mwenye uwezo katika wakati muafaka katika mechi zote tutakazozicheza na siyo kingine, sitaangalia ukubwa wa jina," anasema Brandts.
mwisho

No comments:

Post a Comment