Search This Blog

Wednesday, November 27, 2013

ZANZIBAR HEROES YACHINJA - WAIPIGA SUDAN NA KUONGOZA KUNDI - KENYA NA ETHIOPIA ZATOKA SARE

Zanzibar Heroes imeanza nzuri kampeni yake ya kugombea kombe la GOtv Cecafa Senior Challenge Cup baada ya kuifunga timu ngumu ya South Sudan 2-1 katika mchezo mgumu wa ufunguzi wa michuano hiyo katika uwanja wa Nyayo National Stadium.
Heroes walihitaji dakika 5 tu kupata bao la kuongoza kupitia  Suleiman Kasim.  
Zanzibar waliongeza bao lao la pili katika dakika ya 67 wakati mchezaji aliyeingia akitokea benchi Adeyum Saleh Ahmed alipofunga bao zuri kwa shuti kali lilomshinda golikipa Juma Jinaro.
Japo walikuwa nyuma kwa mabao mawili, Sudan waliweza kujikaza na kufunga bao la kufutia machozi katika dakika ya 75 kupitia mchezaji wao Fabiano Lako. Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Zanzibar waliweza kuondoka na ushindi ambao umeweza kuwafanya kuongoza kundi lao baada ya wenyeji Kenya kutoka sare ya bila kufungana na Ethiopia. 

1 comment:

  1. ALLAH AJAALIE MECHI YA KESHO IPATE MSHINDI MNONO WA MAGOLI MATATU KWA BILA KWA UWEZO WAKE ALLAH MWINGI WA REHEMA

    ReplyDelete