Search This Blog

Saturday, September 1, 2012

AKUFFO NA KEITA: VISU VIPYA VINAVYONOLEWA NA MILOVAN MAFICHONI ARUSHA


MICHAEL MOMBURI, ARUSHA
KUNA watu wawili wako Simba ambao mashabiki wengi wa soka hususan wa Dar es Salaam hawajawaona. Watu hao walitua Dar es Salaam wakakaa siku chache kisha Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic akafanya uamuzi mgumu kuwapeleka porini.

Aliwapeleka kwenye pori la mibuni Arusha linaloitwa Krein Down. Unaingia ndani umbali wa dakika kama 10 kutoka Barabara Kuu ya Arusha-Monduli katika eneo la Kisongo.

Ndani ya eneo hilo kuna uwanja mzuri wenye nyasi safi, upepo mwanana na hakuna raia wanaoruhusiwa kuingia zaidi ya Simba na raia wa kigeni ambao wako makambini maeneo hayo wakijiandaa kwenda kutalii porini.

Watu hao wawili ambao Milovan amewaficha huko ni beki raia wa Mali, Komanbilli Keita na straika Mghana Daniel Akuffo.

Hakuna shabiki wa Dar es Salaam aliyeyaona majembe haya mapya ya Simba na pengine siku yakionekana Uwanja wa Taifa itakuwa balaa.

Wachezaji hao hawazungumzwi sana, lakini wamefiti ndani ya Simba na wanafanya kazi ambayo mchezaji yeyote wa kigeni anastahili kufanya.

Keita amefuta matatizo ya Simba kwenye ulinzi huku Akuffo akiongeza vitu adimu kwenye fowadi ambavyo pengine vinaweza kufanya mashabiki wasahau kelele na siasa za soka la mjini.

KEITA
Ni kijana mdogo wa Mali mwenye umri wa miaka 24 ambaye anazungumza Kingereza kwa taabu kidogo lakini shughuli yake ni nyingine.

Ni fundi wa mipira ya juu, krosi, ametulia, ana nguvu na anatumia akili kabla ya kufanya uamuzi.

Mastraika wa Simba wanamwogopa kwa kitu kimoja, anachapa sana viatu kisirisiri na ukimwingia vibaya siku yako inaweza kuwa imekwisha.

Keita anayezungumza Kifaransa alicheza kwenye klabu maarufu ya Stade Malian kwa miaka saba kabla ya kuhamia Jeanne Dare Arc ambako ndiko Simba ilikompata kupitia kaka yake ambaye ni wakala aliyeko Dubai.
Kaka yangu aliponipigia simu kwamba nenda Tanzania kafanye majaribio nilimshangaa sana. Nikauliza mara ya pili Tanzania? Wewe una matatizo, kuna soka gani huko?

Nilisema vile kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusiana na soka ya hii nchi, alisema Keita mwenye rasta kama Amri Kiemba.

Anaongeza: "Lakini nilipofika Simba nimefuta kauli yangu. Nimegundua kwamba ni sehemu ambayo haina tofauti na Mali, kuna wachezaji wenye vipaji vikubwa na wanaocheza mpira wa pasi na nguvu.

Sizijui klabu nyingine lakini ukiangalia wachezaji kama Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Chombo, Haruna Moshi, Shomari Kapombe na wachezaji wengine inatosha kujua kwamba Tanzania iko vizuri.

�"Nilipomwona Ngassa siku ya kwanza vurugu zake nilishangaa sana, inahitajika akili za ziada kwa beki kucheza na mchezaji wa aina yake.

Si mchezo. Ushindani ni mkubwa sana ndani ya Simba ndiyo maana nimeridhia kusaini kwa kuwa napenda timu inayocheza soka la nguvu, pasi kwa spidi na staili ya Simba.

Ni timu ambayo kila mchezaji yeyote atapenda kuchezea,� anasema mchezaji huyo aliyechezea timu ya taifa ya vijana ya Olimpiki mwaka 2004.

Inabidi kufanya mazoezi ya nguvu sana kumshawishi kocha kwa vile namba yangu ina wachezaji wenye uwezo na waliozoweleka kama Kapombe na Nyosso, lakini wanaojua historia yangu wanajua mimi ni mtu wa kazi muda wote na napenda mechi ngumu kwa vile ndiyo zinanijenga na kunisafishia njia.

Kwa kuwa malengo yangu ni kucheza misimu miwili kwa kiwango cha juu ninyooshe njia yangu nipae Ulaya.

�Naamini Mungu amenileta Simba kwa makusudi ili nipite kuelekea kwenye mafanikio. Nimependa sana staili ya kocha Milovan anachezesha timu kwa staili ya soka ambayo ninaipenda, yaani timu inachezea sana mpira kwa haraka,� alisema shabiki huyo wa Manchester United na Real Madrid.

Akizungumzia tofauti ya Tanzania na Mali anasema:

Mali hakuna timu kubwa, zote ziko kawaida na kila timu inashinda mchezo si kama Tanzania ambapo klabu tatu ndiyo zinaongoza halafu kule kuna akademi nyingi za soka."

AKUFFO

Amecheza mechi mbili na kufunga mabao mawili tena ya kwanza lakini amekuwa akichezeshwa dakika 50 kutoa nafasi kwa wachezaji wengine. Ni straika mrefu kwenye futi 5.8.

Uchezaji wake hautofautiani na Emmanuel Okwi lakini yeye ana shabaha zaidi, haogopi, ana kasi, anakaba na anajua kujiweka kwenye nafasi.

Ni Mghana aliyechezea klabu za Hearts of Hoak, New Edubiase kabla ya kwenda Stella Club ya Ivory Coast ambako ndiko alikotokea akaja Msimbazi.

Kabla hajaja Tanzania alikuwa anajua mambo mawili tu kwamba kuna klabu kubwa za Simba na Yanga na lugha inayotumika ni Kiswahili.

�Nilitarajia kukutana na ushindani mkubwa sana wa namba kwa vile niliifuatilia Simba kwenye mitandao nikaangalia rekodi zake, nimependa sana mazingira ya kirafiki yaliyopo kwani sikutarajia kwamba ningeweza kujenga urafiki na wachezaji kwa kipindi kifupi hivi.

�Wachezaji ni wakarimu sana ndiyo maana unaona kazi yangu inakuwa rahisi, nimefunga mabao mawili kwenye mechi mbili nilizocheza hiyo haimaanishi kwamba nimekuwa fiti sana lakini ni mwanzo wa safari yangu.

Nitacheza sana kwenye ligi, sijajiwekea malengo kwamba nifunge mabao mangapi lakini nitataka kufunga kila mechi.

Ili kunyoosha njia ya yangu, kwavile sehemu nilipo kuna mastraika wengi kama Abdallah Juma, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu na wengine wengi ambao wako fiti kucheza.

�Ili kupata namba na kuitendea haki klabu na mashabiki lazima ufanya kazi ya ziada uwanjani, ninachoahidi ni nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja, kufanya kazi kwa nguvu kupitia malengo ya klabu na kuwaheshimu mashabiki.

Akuffo ambaye anacheza namba zote kwenye fowadi, anaitamani Taifa Stars: �Natamani sana kupata namba ya kuichezea Tanzania kwa kuwa naona kabisa kwamba nina uwezo wa kuisaidia ikafika mbali na ni sehemu tulivu ambayo nitafanikiwa zaidi kwa kucheza timu ya Taifa na klabu kubwa kama Simba.

�Hayo malengo yapo na nitauonyesha umma wa Watanzania kwa vitendo kwamba nina uwezo wa kuvaa jezi ya timu yao ya Taifa na kuwafanyia kazi, Akuffo ni mtu wa vitendo zaidi si maneno.

�Nimecheza timu yangu ya taifa ya vijana U-17 mwaka 2005, ninapenda sana soka la nguvu na ushindani na uzuri ni kwamba sina rekodi ya majeruhi ingawa ni kitu kinachoweza kumtokea mchezaji wakati wowote.

Naitaka Tanzania haimaanishi kwamba Ghana hakuna amani lakini napenda kucheza soka kwenye mazingira ninayopewa nafasi, ukiangalia timu yetu imejaa wachezaji wengi wa Ulaya,� alisisitiza mchezaji huyo anayetumia simu ya kisasa aina ya Samsung Galaxy.


KOCHA MILOVAN
�Mpaka sasa nimeridhika na uwezo wa wachezaji hawa, ni watu wanaojituma sana na ambao nadhani msimu huu wataibadili sana Simba.

Ukianzia na Keita ameongeza kitu cha ziada pale kwenye ulinzi amefuta tatizo lililokuwapo, anaweza kucheza vizuri na Ochieng (Paschal) hata Juma Nyosso.

�Akuffo ni mwepesi na amefanya vizuri katika mechi alizocheza ndiyo maana unaona anafunga kila anapocheza.

Story kutoka Gazeti la Mwanaspoti

No comments:

Post a Comment