Search This Blog

Saturday, September 1, 2012

FIESTA 2012 ILIVYOTINGISHA MUSOMA - YATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA


Bofya hiyo video uone jinsi palivyokuwa hapatoshi ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipokuwa linaunguruma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
 Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
 Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
 Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
 Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Kati ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mwasiti akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
Mmoja wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Rachel (kushoto), akionyesha uwezo wake katika uwanja wa Karume mjini Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 na wanenguaji wake.
Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.



div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">


Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakiongozwa na baadhi ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group wakiwa katika picha ya pamoja jioni ya leo na watoto wanaolelewa  na kituo cha watoto Yatima/waishio katika mazingira sambamba na walezi wao kiitwacho Jipe Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akishiriki kukabidhi sehemu ya msaada kwa niaba ya wasanii wenzake kwa baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo hicho,kushoto ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group akikabidhi pia sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo kwa walezi wa kituo hicho,kilichopo Musoma Mjini.
Mratibu Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo akitoa mkono wa shukurani kwa ujio wao kwa baadhi ya Wasanii  mahiri wa hip hop hapa Bongo Prof. Jay na Fid Q . 
Afisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Simalenga akizungumza machache kwa niaba ya Kampuni na pia kwa wasanii aliombatana nao,katika suala zima la kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo hicho mapema leo jioni,kulia kwake ni Mratibu Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo na kushoto ni Mratibu wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa Kuyenga.
Mratibu wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa Kuyenga akiwakaribisha vyema baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Clouds Media Group na Wasanii walioambana nao jioni ya leo,akiwemo Prof Jay,Fid Q,Chege,Mwasiti,Bibi Cheke,Omy Dimpo,Bob Junior,Roma,Barnaba na wengineo. 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakiongozwa na mkongwe wa muziki wa Bongofleva,Prof Jay wakitia saini kitabu cha wakati,mara walipowasili kwenye kituo cha Jipe Moyo Center jioni ya leo,wasanii hao watatumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo kesho pia watakamua kwenye uwanja wa Kambarage,mjini Sinyanga. 
Mmoja wa wasanii anaekuja kwa kasi katika anga ya bongofleva,Ommy Dimpo a.k.a Pozi kwa Pozi akijitambulisha mbele ya wenyeji,ambapo wageni wote wakiwamo wasanii walijtambulisha.
  Mkongwe kwa umri lakini anakamua vilivyo kwenye anga ya bongofleva,Bibi Cheka nae akijitambulisha mbele ya wenyeji.
 Sehemu ya misaada kama inavyoonekana mara baada ya kukabidhiwa kwenye kituo hicho.
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiwasili kwenye kituo cha kulelea watoto Yatima/waishio katika mazingira magumu kiitwacho Jipe Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment