Search This Blog

Friday, February 14, 2014

KIUFUNDI: FOMU MBOVU YA ARSENAL DHIDI YA TIMU KUBWA INAIGHARIMU NDOTO YAO YA KUMALIZA UKAME WA MIAKA 9 WA UBINGWA

Msimu uliopita Arsenal ilimaliza msimu ikiwa kwenye kiwango cha juu, ikishinda me chi mfululizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki Champions League. Jambo moja ambalo limekuwa likiangusha Arsenal kwa misimu kadhaa iliyopita - ni kupata point chache kutoka vilabu vyenza vya Top 4. Arsenal ilichukua jumla ya point 2 tu kati ya 18, walifungwa me chi 4, wakitoa sare mara mbili na hawakushinda mchezo hata moja dhidi ya Man United, Chelsea, na Man City. Je hii inajirudia pia msimu huh na itaigharimu Arsenal na ndoto yake ya kutwaa ubingwa?

Kama tunavyoona hapo juu fomu ya Arsenal dhidi ya vilabu vinavyoshika nafasi za juu msimu huu ni sawa sawa tu ilivyokuwa msimu uliopita. 
Liverpool, ambao wamefungwa mechi zao 3 za ugenini dhidi ya timu za juu, ina pointi 3 tu kutoka kwenye mechi dhidi ya timu za Top 4, pointi hizo imezipata kutka kwa Arsenal. Jambo la kusikitisha zaidi pamoja na msimu huu kujirekebisha kidogo kwenye ulinzi lakini Arsenal imeruhusu mabao 11 kwenye mechi mbili dhidi ya Manchester City na Liverpool. Hili ni jambo la kutia wasiwasi.

Kuna wasiwasi au mtazamo kwamba timu haijiandai vizuri na michezo dhidi ya timu kubwa, wanaruhusu mabao mengi. Jambo lingine la kutia shaka safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao manne tu, namba ndogo zaidi miongoni mwa mechi za timu za top 4. Chelsea wana rekodi nzuri, wameruhusu mabao 3 tu na ndio timu pekee iliyoenda Etihad na kushinda - na kutoka na clean sheet pia. 
Manchester City wana kikosi kizuri mno na itakuwa vigumu kufungwa watakapoenda Emirates na Anfield. Chelsea wana mchezo mmoja wa ugenini dhidi ya Liverpool na mmoja wa home dhidi ya Arsenal. Fomu ya Chelsea dhidi ya timu za juu ni nzuri sana na chini ya Jose Mourinho  wameweza kujua namna ya kupata matokeo katika mechi kubwa kwa mbinu zozote zile. 
Wenger inabidi ajipange vizuri katika mechi mbili zijazo dhidi ya Manchester City na Chelsea, endapo watapoteza mechi hizo ni wazi ndoto yao ya kubeba ubingwa msimu huu itabaki kuwa ndoto. 
Arsenal wana mkusanyiko wa michezo migumu sana katika siku za hivi karibu. Jana walishindwa kuifunga Man United walio kwenye hali mbaya kabisa, wakitoka hapo wanaenda kukutana Liverpool kwenye kombe la FA, then wanaikaribisha Bayern Munich Emirates wiki ijayo, then watakutana na mahasimu wao Spurs, na Chelsea kisha Everton, huku wakisubiri kuikaribisha City Emirates. 

Mpaka kufikia mwishoni mwa 3 tunaweza kujua hatma ya Arsenal msimu huu - watamaliza ukame wa miaka 9 bila kombe au wataingia mwaka wa 10 bila kuvaa medali.

No comments:

Post a Comment