Search This Blog

Friday, February 14, 2014

TWIGA STARS YATUA LUSAKA, YAAHIDI MAPAMBANO

Kikosi cha wachezaji 19 wa Twiga Stars kimetua Lusaka, Zambia leo
(Februari 13 mwaka huu) huku Kocha Mkuu Rogasian akiahidi ushindani kwenye
mechi dhidi ya wenyeji itakayochezwa Uwanja wa Nkoloma.

Kocha Kaijage aliwaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kenneth Kaunda mara baada ya kikosi chake kutua kwa ndege ya
Fastjet saa 3.30 asubuhi kwa saa za Zambia kuwa wamekuja kushindana, na si
kushiriki.

Twiga Stars ambayo mara ya mwisho ilikutana na Zambia kwenye michuano ya
COSAFA miaka miwili iliyopita na kuibuka na ushindi imefikia hoteli ya
Golden Peacock, na katika uwanja wa ndege ilipokewa na viongozi wa Chama
cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ) na Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini
Zambia, Jeswald Majuva.

Timu hiyo leo saa 9 alasiri kwa saa za Zambia ambapo Tanzania ni saa 10
jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nkoloma ambao ndiyo utakaotumika
kwa mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC)
itakayochezwa kesho.

Wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho ni Amina Ali, Anastazia Katunzi,
Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine
Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari,
Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwapewa Mtumwa, Sherida Boniface,
Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.

No comments:

Post a Comment