Search This Blog

Wednesday, February 12, 2014

ARSENAL VS MAN UNITED - MAJERUHI WAWILI WANAPOGOMBANIA TIBA YA USHINDI USIKU WA LEO EMIRATES. NANI KUPONA?


Arsenal inaikaribisha Manchester United katika mchezo ambao ni muhimu kwa timu zote mbili.Mechi hii kawaida ni mechi inavuta hisia za mashabiki wengi duniani bila kujali vilabu vipo kwenye hali gani lakini ukifikiria matokeo ya wikiendi iliyopita, mchezo huu unazidi kuwa muhimu zaidi.
Arsenal wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kipigo kitakatifu cha 5-1 kutoka kwa Liverpool jumamosi iliyopita. Majogoo wa jiji waliipiga Arsenal 4-0 ndani ya dakika 20 tu, kitu ambacho itabidi Gunners wakiwekee umakini ili wasikutane nacho katika mchezo wa leo.Huku mbio za ubingwa zikiwa zimepamba moto, Arsenal leo wanahitaji kushinda ili warudi kileleni vinginevyo wanaweza kujikuta wakizidi kuteremka chini kwenye msimamo. Matokeo ya wiki hii hayakuwa mazuri kabisa ukizingatia ratiba ngumu waliyonayo. Baada ya kucheza na United leo, Arsenal watakutana tena Liverpool lakini safari hii kwenye FA Cup, baada ya hapo watacheza na Bayern Munich katika Champions League. 
Man Utd kwa upande mwingine wapo katika nafasi ya saba, wakitoka kutoka sare ya 2-2 na Fulham wanaoshika nafasi ya mwisho kwenye ligi. Ilikuwa ni mechi ambayo United ilishambulia sana, lakini wakakosa makali kwenye lango la wapinzani na mwishoni wakaonjeshwa utamu wa dawa yao wenyewe kwa kuruhusu bao la dakika ya mwisho kabisa ya mchezo na kupoteza pointi mbili muhimu. Huku matumaini yao ya kucheza Champions League yakianza kupotea, matokeo ya wikiendi yaliwafanya kuwa nyuma kwa pointi tisa kutoka kwa wanaoshika nafasi ya nne Liverpool, ambao pia wana wastani mkubwa wa mabao. United watakuwa na matumaini ya kurudisha utamaduni wao wakati Sir Alex Ferguson alipokuwa kocha, huku wakiomba timu nyingine zinazogombea nafasi ya nne za juu zipatae matokeo mabaya.
Mechi ya Arsenal vs Man Utd siku zote imekuwa na upinzani mkubwa kuanzia miaka ya mwanzoni miaka ya 2000. Timu hizi mbili zimekuwa zikigombea ubingwa zenyewe kwa zenyewe na upinzani wao ulikuwa ukionekana wakati wa mechi zao. Enzi za ugomvi wa Viera na Roy Keanezimepita lakini upinzani bado upo. Huku usajili wa Van Persie kutoka Arsenal kwenda Old Trafford, imezidisha uhasama miongoni mwa mashabiki, hasa zaidi baada ya Van Persie kufunga mara kadhaa dhidi ya Arsenal tangu ajiunge na United, likiwemo bao la ushindi katika raundi ya kwanza. 

Habari za Timu

Arsenal

Arsenal walikosa ubunifu na walikuwa wepesi kwenye kiungo siku ya jumamosi huku pengo la Flamini likionekana wazi. Kiungo huyo wa kifaransa anatumikia adhabu ya mechi 3 hivyo kwa mara nyingine atakosekana kwenye mchezo wa leo. Mchezaji mpya Kim Kallstrom ni majeruhi kama ilivyo kwa Walcott na Diaby. Vermaelen anakaribia kurejea lakini sio rahisi kucheza kwenye mchezo huu, Ramsey atakuwa nje mpaka mwezi ujao. Wenger anategemewa kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza huku Gibbs, Rosicky  NA Podolski wote wakitegemewa kuanza. 

Man United

Phil Jones anaweza kurudi kwenye kikosi cha kwanza cha United mara baada ya kurudi kutoka kwenye majeruhi. Fellaini, Nani na Ferdinand wote watakuwa nje kwa pamoja na Cleverley na Evans ambao walipata majeruhi hivi karibuni. 

Vikosi vinavyoweza kuanza

AFC vs MUFC 529x410 Arsenal vs Manchester United Preview | Team News, Key Players, Stats

Takwimu mbalimbali za kuvutia

  • Gunners wameshinda mechi zao sita kati ya nane zilizopita za Barclays Premier League walizocheza nyumbani kwa mabao 2-0. 
  • Arsenal wameshinda mechi moja tu kati ya 10 za premier league dhidi ya Arsenal (W1 D2 L7).
  • Hii ni mara ya kwanza Arsenal na Manchester United zinakutana kwenye Premier League baada ya kushindwa kushinda kwenye zao za nyuma tangu April 2008.
  • Arsenal wameweza kuwa na clean sheets 10 katika mechi 11 zilizopita katika mashindano yote ndani ya dimba la Emirates. 
  • Robin van Persie amefunga katika mechi 5 zilizopita za premier league baina ya timu hizi mbili - mabao 3 kwa United - mabao mawili kwa Arsenal. 
  • Wayne Rooney amefunga mabao 10 ya premier league dhidi ya Arsenal. ndio mchezaji anayeongoza kufunga mabao mengi katika historia ya timu hizo mbili. 

No comments:

Post a Comment