Search This Blog

Thursday, February 13, 2014

UMRI WA MCAMEROON WALETA GUMZO BARANI ULAYA: ADAI ANA MIAKA 17 - SHIDA ZA KIMAISHA UTOTONI ZIMEMKOMAZA


Moja ya story kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka wiki hii inamhusu mchezaji mpya wa klabu ya Lazio, Joseph Minala, ambaye watu wengi wamekuwa na mashaka na umri sahihi wa kiungo huyo wa Cameroon kwamba ana miaka 17 au 40 na zaidi.

Kulikuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, akionekana kukasirishwa na kejeli na matusi ya mashabiki Joseph Minala aliamua kujibu mapigo kwa ujumbe wenye maneno makali kupitia akaunti yake ya Twitter kabla ya kuifunga, pia akaifunga ya Facebook na kuiweka ya instagram private.

Wakala wake Diego Tavano nae amezungumzia suala hili huku akimtetea mteja wake kwamba "shida za kimaisha" zimechangia muonekano wa kiutuzima wa mteja wake. Akiongea na Gazzetta dello Sport alisema: "Suala la Joseph Minala lipo wazi. Alikuwa amelelewa kwenye mazingira ya shida sana wakati wa udongo wake, hali iliyopelekea muonekano wake huu wa hivi sasa."

Mmiliki wa klabu iliyomuuza kwenda Lazio, bwana Mauricio Perconti, nae alimtetea: "Siwezi kukataa kwamba anaonekana mtu zima sana, lakini vielelezo vyote vinaonyesha umri wake ni miaka 17."


TAZAMA PICHA ZA MINALA KISHA TOA MAONI YAKO. UNADHANI ANA MIAKA 17 KWELI?
BgR 1SJCEAEbzPz Joseph Minalas agent says his 17 year old client who looks 40 appears older because of a difficult childhood
BgDmZIgIgAAbpp2 Joseph Minalas agent says his 17 year old client who looks 40 appears older because of a difficult childhood


10 comments:

 1. Duh huyu sio wa miaka 17 wamepitiza uongo hata ukimuweka na kapombe mwenye umri 21 anaonekana tu jamaa mkubwa atleast wangesema ana umri wa miaka 27 hv tungemtetea cos ni mwafrica mwenzetu but kum17 ni no no big no.haikubalik ana umri wa matola huyo au kiminyio madaraka suleiman

  ReplyDelete
 2. Wamuingize kwenye vipimo vya mifupa watAjua huyo yuko kwenye 32

  ReplyDelete
 3. du jamaa noma, wakikaa vibaya huyu atafanya surgery aonekane dogo, ila kama ameshinda hiyo vita na akapata timu poa, mmi nina msifu. bora alivofanya kuliko kuuza dawa za kulevya.

  ReplyDelete
 4. jamaa atakuwa na miaka 33 kwan macho yake yanaonyesha kabisa umri ni miaka 33.

  ReplyDelete
 5. Bas angejiweka atleast 22yrs! Lkn cyo 17...

  ReplyDelete
 6. hata kama alipitia maisha ya ziki ndio siyo kihivyo

  ReplyDelete
 7. U-17 ya Africa balaaa! Ndio maana wanachukua makombe ya Dunia ya vijana lakini ya wakubwa Du! Subiri apate majeraha na kupangiwa dozi ya mtoto ndo utakuwa mwisho wake

  ReplyDelete
 8. duh hata mimi siamini km ana umri wa miaka17, huyo ana zaidi ya 27,

  ReplyDelete
 9. majanga,mbona majanga

  ReplyDelete