Search This Blog

Wednesday, July 31, 2013

MAKALA: DILI LA AZAM MEDIA NA LIGI YA TANZANIA - SUPERSPORT NA ASILI YA SOKO LETU.



Wiki iliyopita kamati ya ligi ya VPL na TFF ziliingia mkataba na kampuni ya Azam Media Group kwa kuwauzia haki za matangazo ya Television kwa ajili ya kuonyesha ligi kuu ya Tanzania bara.

Pia zilitoka ripoti kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari kwamba kampuni nyingine kutoka nje ya Supersport ilionyesha kuvutiwa na dili hilo lakini ikashindwa na Azam Media ambao walitoa ofa kubwa zaidi. Hii ni habari ngumu kuiamini kwa kuzingatia hakuna mtu yoyote anahusika aliyethibitisha kama kweli
SuperSport walitoa ofa rasmi ambayo ilizidiwa na wapinzani wao.

 Tena ukiangalia uzoefu na ubavu wao wa kifedha na teknolojia katika uonyeshwaji wa michezo  kwenye upande wa kusini mwa jangwa la Sahara, ni vigumu kuamini wangeweza kushindwa kirahisi kama kweli walikuwa wanahitaji kwa nia ya dhati kuonyesha ligi ya Tanzania. ukiliangalia Hili kwa mtazamo wa kibiashara zaidi utagundua kuwa kwenye nchi za Kenya na Uganda wana watumiaji wengi wa DSTV, Kenya wakiwa na asilimia 44 na Uganda 28, ukilinganisha na asilimia 12 ya Tanzania. 

Kwa maana hiyo Tanzania imekuwa na wateja wachache wa huduma za DSTV, na wengi wao wanatumia kwa kuangalia mchezo wa soka, tofauti na nchi za Uganda na Kenya.


 Kenya na Uganda wote wanashiriki kwenye michezo tofauti, rugby na riadha ambayo yote inaonyeshwa. Tanzania mchezo wetu mkuu ni soka, na michezo mengine hata kama ipo lakini haina dili kubwa kwenye masuala ya kuuza haki za matangazo ya TV. DSTV kama wangeamua kuja kuonyesha soka hapa Tanzania, basi uwekezaji wao mkubwa wa vifaa ungewagharimu zaidi ikizingatiwa ni soka tu ambalo wangeonyesha kwa maana kipindi kingine wakati ligi imesimama mitambo yao isingekuwa inatengeneza fedha za ziada - tofauti na nchi za Uganda na Kenya ambao muda wote inakuwa inafanya kazi kutoka na wingi wa michezo tofauti inayoonyeshwa kutoka kwenye nchi hizo.

Azam Media wanaweza kuwa wametoa ofa nzuri ya kifedha lakini kama Supersport wangetaka kweli kuonyesha umwamba wao wa kiuchumi, basi ingekuwa vita nzuri ya kibiashara - ambayo ingeviacha vilabu vyetu vikienda benki huku vinatabasamu. 

Wakati GTV ilipotaka kuchukua haki za matangazo ya Kenya Premier league, SuperSport waligundua walikuwa wanapoteza kitu kikubwa sana kibiashara. GTV tayari walikuwa wameshakamata haki za matangazo ya ligi za Uganda na Tanzania na walikuwa wakitaka kumalizia na Kenya. Hivyo Supersport wakalazimika kuja na ofa nzuri zaidi na mwishowe wakafanikiwa kushinda tenda ya haki za matangazo za KPL. Hivyo ndivyo ushindani wa kibiashara ulivyo. 

Ingekuwa SuperSport wanataka kweli na kuona kuna fursa ya kibiashara kuja kuwekeza kwenye ligi ya Tanzania basi wangeweza kutoa ofa nzuri zaidi waliyotoa Azam Media Limited. Lakini pia, kamati ya ligi ingeweza kufanya kazi nzuri zaidi kama wangetangaza tenda ambayo ingevutia media tofauti kuja kushindana kwa kutoa ofa tofauti. 

Ni vigumu kupata dili zuri zaidi ya walilitoa Azam Media limited ukiangalia na asili ya soko letu. Ambalo ni dogo na limejitenga kiasi kuwa na uwezo mdogo wa kuvutia Media kubwa kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza kama ambavyo Azam wameweza.  

Pia kama taratibu zote zingefuatwa, labda klabu zetu zingeweza kupata fedha nyingi zaidi kutokana na ushindani wa makampuni ambao ungekuwepo kugombea tenda hiyo. Lakini katikati ya maneno maneno yaliyojitokeza katika dili hili - tusisahau kwamba Azam wametoa nafasi kwenye mkataba kwa media nyingine kushirikiana nayo.

Azam kwa kutokuwa wabinafsi inasemekana waliamua kisiwepo kipengele ambacho kingefunga njia kwa wawekazaji wengine ambao wangetaka kushirikiana nao. Kwa mfano Zuku , StarTimes au SuperSport kirahisi tu wanaweza kushirikiana kibiashara na Azam katika kurusha matangazo hayo ya mechi za ligi kuu. Kwa kifupi, Azam TV hawajabana milango kwa wengine kwa maana ya 'exclusive rights', kuna nafasi kubwa ya Media nyingine zitakazojisikia kushirikiana nao kwa makubalianao watakayokubaliana.

Japokuwa dili bado dogo kwa baadhi ya vilabu vyenye bajeti kubwa, lakini bado ni tamu kwa vilabu vyenye bajeti ndogo japokuwa ni vigumu kuacha kuyasemea makosa yaliyofanywa na kamati ya ligi pamoja na TFF ya kutaka kulazimisha kusainisha mkataba na Azam Media.  
Story hii imeandikwa na ALLEN MICHAEL wa lonestrikertz.blogspot.com

15 comments:

  1. acha umbea kijana kuna mambo ya kuangalia,nilikuwa nakuamini kumbe mbabaishaji,tunachoshaa leo vilabu vinafufaika tunapiga kelel,wakati super sport wanaonyesha bure tumepika kelele,naimani AZAM co,c wababaishaji,natumai Insh Allah tutafika cku 1

    ReplyDelete
  2. simba sc vs clouds media simba wameilipa clouds media
    simba sc tv nvs Azam Tv Azam tv wameilipa simba

    Shaffih Dauda =clouds Media group=mgongano wa maslai
    Acha unafki katika hili

    Mdau Lamadi- Simiyu

    ReplyDelete
  3. Shaffih aliyekuambia supersport wana ubavu kifedha kushinda AZam Media ni nani? Acha ku guess

    ReplyDelete
  4. Ww shaffi huelewekii unabwabwaja tu maeneno,hao supersports ni mara ngapi wameonyesha michezo hiyo eti kwa kisingizio cha promo,kila kitu kinamwanzo kama Azam wameonesha nia ya dhati basi wapewe lakin hizi timu za simba na Yanga kweli ni pesa kidogo kwa hadhi yao maana wakicheza wenyewe tu ni zaid ya 100mil

    ReplyDelete
  5. Jibuni hoja.tuache kuona huruma.hapa ni suala la kibiashara zaidi si soka kama azam inavyojitanabaisha mpira wa bongo unawapenzi wengi wa yanga na simba sasa azam wanawataka wapenzi hao kwa ajili ya biashara. Sasa yanga imejitambua isitumike kama punda kwa ajili ya kuvisaidia vilabu vingine na biashara za azam hivyo yawapasa azam kuisikiliza yanga nn inataka au yanga iruhusiwe kutafuta tv yake kwa manufaa yake au yenyewe na baadhi ya timu.Simba ni wanafiki vigeugeu kwa mkataba tu na azam tayari wamepata zaidi lkn kwa ulimbukeni watatumika zaidi kwa faida ya wanyonyaji na walafi azam.

    ReplyDelete
  6. nikweli kbs mate(shaffih),mie wasiwasi wangu mkubwa ni jinc hyo kamati ya mpito inavyokuwa inaforce deal ifanyike fasta fasta wkt kamati yenye haki itachaguliwa very soon tena kwa kupigiwa kura.isitoshe hyo Azam tv sijui inapatikana channel number ngapi?ata ubora wa hyo channel aujulikani wakati ligi inatakiwa kuanza next three weeks..Haya mambo ni ya ajabu sana watu wanatakiwa wabadilike,pia 100mil aitoshi kwa Yanga mkumbuke hao simba wameingia mkataba na hao azam kwa ajili ya simba tv wa sh 300mil miaka 3 hapo unaweza ukaona kwanini hao simba wamekaa kimya kwa hilo swala.

    ReplyDelete
  7. Super sports hawana mana wanatudharirisha tu kwa kuonyesha mechi bure wakati Kenya na Uganda wanalipa.

    Safi sana Azam Media

    ReplyDelete
  8. kuna mtu kauliza Hivi ofisi za Azam Tv ziko wap, coverage yake ikoje, picture quality yake ipo vp, inarushwa kwa kingamuzi gani, Watangazaji wake wanauwezo gani???

    ReplyDelete
  9. Waacheni azam media group wafanye kazi tione
    Tusamin vya nyumban kwanza
    Kwani ht supersport haikujengwa siku moja

    ReplyDelete
  10. huyu shaffi bure kabisa, labda kama anapiga kelele kwa manufaa binafsi lakini haiingii akilini kupinga huo mkataba wakati vodascom haitoi pesa zote hizo, vilabu vinaendeshwa kwa shida sana, matokeo yake ni kuuza mechi au wataka tuwe huko? kila kitu kina mwanzo, pia unapowatetea yanga, je mkataba wao na TBL uliwekwa kwenye zabuni?

    ReplyDelete
  11. Duuuuh! Hili linapaswa liwekwe kwenye historia, hiyo Azam media iko wapi ama ndiyo ile tv show ya channel ten itaonesha ligi kuu! Hamna mgongano wa maslahi wala nn, waanze kwanza kazi tuwaone na uchaguzi wa TFF ufanyike ili wenye mamlaka ya kusaini mkataba wafanye kazi yao kwa kuzingatia taratibu zote za mikataba na maslahi ya kila mdauu!

    ReplyDelete
  12. Hapa nimegndua kwmba kuna mijitu ina chuki bnafs na clouds na watangazaji wake,manake habari imeandkwa na mtu mwngne toka blog nyngne,lakn analaumiwa Shaffih Dauda! Mambo gani haya jamani,af mawazo ya mtu yaheshmiwe,jifunzen kutoa critics kwa hojaaaaaaa!

    ReplyDelete
  13. Nashkuru kwa taarifa yenyemwangaza haswa upande wa data za watumiaji wa DSTV naona ni factor ya ukweli katika maamuzi. Ila nyumbani ni Nyumbani tuone na tuwa tayari kujaribu tunaogopa nini? Kila mtu anapigia debe vya nje. Kila timu inapaswa kujitambua na huu ni mwanzo na mkataba sio exclusive sasa kele za nini tuone. Asante Shafii

    ReplyDelete
  14. Kwa taarifa zisizo rasmi, Azam TV itakuwa ikipatikana kwenye king'muzi cha star times na DSTV, nadhani kwa hapo coverage ya ligi itakuwa kubwa hasa ukitegemea bajeti ya marketing ya ligi wameweka kubwa

    ReplyDelete
  15. Azam tv itapatikana kwenye king'amzj chao kinaitwa AZAMTV ni dish satelite kwa tuliotembelea kwwnye maenysaho ya sabasaba tuliona na aakasema watakuwa na vitu mbomba zaidi kama dstv.

    ReplyDelete