Search This Blog

Saturday, August 3, 2013

SIMBA YAENDELEZA BALAA KWENYE USAJILI - YAMSAINI RASMI BEKI WA KATI NAHODHA WA TIMU YA TAIFA YA BURUNDI GILBERT KAZE

Klabu ya Simba imekamilisha rasmi usajili wa beki wa kati Gilbert Kaze kutoka Vital O ya Burundi. Gilbert aka Demunga ni mmoja wa mabeki bora walionyesha kiwango kizuri hasa kwenye michuano ya Cecafa iliyopita. Amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba. Gilbert Kaze pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Burundi - na alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa timu hiyo walioiwezesha Burundi kufuzu kucheza CHAN mwakani nchini South Africa.

12 comments:

  1. Timu za simba na yanga niujinga mtupu wageni kibao kuliko wazama mnakomoana au mnakomoa taifa kuzenu wenu upuzi wa kuchukua wageni tupa kule

    ReplyDelete
  2. vilabu vya simba na yanga ndovinaua vpaji hapa tz

    ReplyDelete
  3. karibu tanzania karibu simba sports club

    ReplyDelete
  4. Godfrey Nyange Kaburu is reaalt missed out there..Huu ni usajili mbovu sijapata ona wanasajili mabeki tu hawa jamaaa...ligi ianze tu match 5 za kwanza rage anatimuliwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mchukue Kaburu wako mkageuzane, wakati yeye kiongozi hao kina Ochieng, Akkufor, A Juma, Kinje, Keita walikuwa wazuri sio, nani kampeleka Yondani Yanga??

      Hizo njaa zenu za kushobokea watu pelekeni kwenye madanguro yenu, Kaburu hajazaliwa kuongoza Simba na kukaa kwake nje sio tatizo bali ni faida!

      Delete
    2. Wewe ndio kichaa Tambwe nae beki?je hujui tatizo la simba mwaka jana lilikuwa nini zaidi? Pia mbona hukusema mwaka jana yanga iliposajili mabeki tu? Je hao maforward waliosajiliwa na simba mwaka huu hujawaona?

      Delete
  5. Makosa ya timu zetu za bongo ni mengi sana kama vile bado tunafikiria tukifungwa tupindue uongozi uliopo madarakani,viongozi ndio wanaofanya usajili badala ya mwalimu. matokeo yake majaribio ya wachezaji tu yanagharimu pesa kibao? halafu timu ikifanya vibaya fukuza kocha pia hatujaondoa dhana kuwa yanva na simba ndio kila kitu katika soka letu

    ReplyDelete
  6. Huu utamaduni wa hizi timu mbili kugombea mchezaji mmoja sijui utaisha lini huko nyuma ilitokea kwa Yusuf Bana timu moja alisajiliwa kama Yusuf Bana na timu nyingine akaitwa Yusuf lsmail ikaja kwa Thomas Kipese mara Ezekiel Junuman na hawa wengine wa hivi karibuni Twite, Yondani hatimae Mosrs Oloya hivi huu ugonjwa gani tunaorithishana naomba tutafute dawa yake ili vizazi vijavyo visalimike nao

    ReplyDelete
  7. Wamepewa Nafasi wazawa wameshidwa Ngoja 2one Owino na Huyo Kaze watapowafundisha jisi mkoba unapomaliza,Yondani mwenyewe alipata ujuzi kutoka kwa Owino.

    ReplyDelete
  8. si sajihi kuwaponda wachezaji wa nje na kikubwa mimi napongeza uwepo wao katika ligi yetu imeleta msisimko mkubwa japo kuwa hatujafika kiwango kinachotakiwa.tunasahau tatizo la wachezaji wa ndani wengi wao ni rajisi kuuza na kuhujumu timu zao tafauti na wa nje wachezaji wetu bado akili zao hazijawaa wazi katika uzalendo wa timu zao mpaka taifa lao wa nje wanajuwa wamekuja kufanya nini wanajali kazi zao wanajali yimu zao ndio maana wenzetu wakiwa nje wanafanikiwa tafauti na wa kwetu mifano iko mingi wengine walipokwenda nje na mpira wakaacha kabisa hawakuona umuhimu wake wengine wakaamua kurudi. wameshindwa kuvumilia hakuna kaburu wala sefu magari wa kuwapa hela bila jasho kwa hiyo wachezaji wetu wamelemaa sana na maisha ya bongo na hao wa nje sio wengi ila ni wa tano na timu zenye. wachezaji wa nje hazizidi tano au sita kwa sasa kwa hiyo hawaathiri wachezaji wa ndani kikubwa wachezaji wetu wabadilkie na wajitume na nidhamu na kuacha misumari mazoezi na bidii ndio siri ya mafanikio

    ReplyDelete
  9. Vital o ni timu ya kawaida bora wangesajili toka Mtibwa kuendeleza soka letu

    ReplyDelete
  10. ndugu yangu tino mandela huna unalo lijua kwenye soka kaa kimya ,unasema yanga na simba wanajaza wageni wengi kuliko wazawa ,hujui kama kila timu mwisho kusajili wachezaji 5 wa kigeni? hizi nafasi zinazo baki ni za hao ndugu zako unaowapigia debe kama ligi ya tanzania imejaa wageni vipi ulaya utasema ? Tatizo si wageni ila wachezaji wako wa tanzania pasua kichwa bado hawaja jitambua

    ReplyDelete