Search This Blog

Saturday, August 3, 2013

VIDEO: HUYU NDIO MOSES OLOYA ANAYEZITOA UDENDA SIMBA NA YANGA KWENYE USAJILI MSIMU HUU - AKIRI TIMU ZOTE ZINAMTAKA

 
HAYA NI MAHOJIANO BAINA YA OLOYA NA GAZETI LA MWANASPOTI
MCHEZAJI wa Xi Mang Saigon ya Vietnam, Moses Oloya amekiri kupokea tiketi ya ndege aliyotumiwa na Yanga, lakini akasema hajachagua timu ya kuichezea kati ya Simba na Yanga. Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Vietnam jana Ijumaa, mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda alisema amefanya mazungumzo na klabu zote mbili; Simba na Yanga lakini atafanya uamuzi wa mwisho Agosti 31 baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Vietnam. “Mkataba wangu unakwisha mwishoni mwa Oktoba, lakini mechi za Ligi Kuu Vietnam tunamaliza Agosti 31,” alisema. Haya ndiyo mahojiano ya Mwanaspoti na Oloya yaliyofanyika jana Ijumaa saa 9:15 alasiri kwa dakika 12. 

Mwanaspoti: Kuna utata hapa Tanzania, ni timu gani unakuja kuichezea msimu ujao? 
Oloya: Ngoja nikuambie ukweli, mpaka sasa sijaamua kati ya Simba na Yanga. 
 Mwanaspoti: Kwani umefanya mazungumzo na timu zote mbili? 
Oloya: Ndiyo karibu kila siku ninazungumza na watu wa Simba na Yanga.
 Mwanaspoti: Umewaambia nini? 
Oloya: Nimewaambia wasubiri nimalizane na timu yangu ya Saigon. 
Mwanaspoti: Utamalizana lini na timu yako ya Saigon? 

Oloya: Tutamaliza mechi ya mwisho ya ligi Agosti 31, lakini mkataba wangu unakwisha Oktoba mwishoni. 

Mwanaspoti: Mbona tunasikia upo Dar es Salaam?
Oloya: Hapana, nipo Vietnam.
Mwanaspoti: Kwa mara ya mwisho umekuja lini Dar es Salaam?
Oloya: Kwa mara ya mwisho nimekuja Dar es Salaam Kombe la Chalenji mwaka jana.
Mwanaspoti: Mbona tunasikia umekuja Dar es Salaam wiki hii?
Oloya: Hapana, nipo Vietnam, tena nipo na Geoffrey Kizito hapa tunakwenda kupata chakula cha jioni (Namsalimu Kizito).
Mwanaspoti: Lakini moyoni unaijua timu utakayochezea msimu ujao?
Oloya: Zipo timu tatu, timu yangu (Saigon) bado wapo fifte fifte, halafu kuna hizo Simba na Yanga. Bado sijajua timu ambayo nitaichezea. Itategemeana na makubaliano.
Mwanaspoti: Mbona tumeambiwa Yanga wamekutumia tiketi ya ndege?
Oloya: Ni kweli, Yanga walinitumia tiketi ya ndege, ambayo ilitakiwa niwe Dar es Salaam Alhamisi na kurudi Ijumaa wiki hii.
Mwanaspoti: Mbona umeshindwa kuja Dar wakati tayari ulitumiwa tiketi na Yanga?
Oloya: Klabu yangu imekataa kuniruhusu, kwa sababu tuna mechi muhimu kesho (leo Jumamosi) dhidi ya Da Nang.

Mwanaspoti: Hiyo tiketi ilikuwa ni ya ndege gani?
Oloya: Qatar Airways
Mwanaspoti: Kwa hiyo ulitaka kuja kusaini mkataba Yanga?
Oloya: Nilitaka kuja kuwasikiliza.
Mwanaspoti: Kwa hiyo mpango wako ni upi kwa Yanga na Simba?
Oloya: Wameniambia nimalizane na klabu yangu (Saigon) na hicho ndicho ninachokifanya, ingawa pia timu yangu bado haijawa wazi kama itanipa mkataba mpya au la.
Maelezo ya ziada
Baada ya mechi ya leo Jumamosi, Saigon itakuwa imebakiza mechi nne dhidi ya Kien Giang, Song Lam Nghe An, Hoang Anh Gia Lai na Long An.
Saigon inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 23 katika msimamo wa Ligi Kuu Vietnam yenye timu 12.
Usajili wa awali wa Ligi Kuu Bara msimu ujao unafungwa Jumatatu saa 6.00 usiku lakini utafungulia tena kwa muda wa wiki mbili kuanzia Agosti 15 na kwamba hadi jana Ijumaa jioni Simba na Yanga zilikuwa na wachezaji wanne wa kigeni kila moja na wanamsubiri mchezaji huyo kujazia orodha yao.

5 comments:

  1. ndo yale yale magazeti yetu lile la jana limepata wapi khabari ile na kama itakua si sahihi mpaka kaandika na kiwango cha.pesa walizotoa yanga kwa ajili hiyo na wakasema viongozi wa yanga wamekwenda kumalizana na club yake ilikuwaje?na kwanini gazeti kama hili halivhukuliwi hatua kwa kuwa limepotosha umma wa wapenda soka na watanzania kwa jumla

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndg yangu magazeti yako kwenye biashara na wanatafuta bidhaa inayohitajika sokoni kwa wakati huo...na si unajua hulka ya biashara nyingi za bongo bidhaa nyingi zinakuwa feki...chukulia habari za magazetini na hasa ya michezo kuwa ni umbea ambao unaweza kuwa kweli au uongo tu..

      Delete
  2. Shaffih,
    Mbona ni mchezaji wa kawaida tu? Anapiga chenga zingine si muhimu kabisa, tena snatufi golini kwake wakati wenzake wame open. Kazi kwa waalim kumbadilisha

    ReplyDelete
  3. huu n upuuz kwa cc kung'ang'ana na mchezaj ambye mwsho wa cku n u2mbo m2pu

    ReplyDelete
  4. Sasa kama mlifanya naye mahojiano mlikuwa hamjui yuko wapi kweli mpka mkamuuliza? yalikuwa mahojiano ya simu au barua? Hamkujua mnazungumza na namba ya nchi gani? au ilikuwa ni skype?

    ReplyDelete