Search This Blog

Wednesday, July 31, 2013

MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUCHEZA MECHI NYINGI ZA KIMATAIFA - AHMED HASSAN AGHAIRI KUSTAAFU

Mchezaji mwenye rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi za kimataifa. Ahmed Hassan, ameamua kutostaafu kwa kuongeza msimu mmoja wa kuichezea klabu ya Misri Zamalek.

Kiungo huyo mwenye miaka 38, ambaye kwa sasa amejiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Misri, atacheza kwenye michuano ya kombe la mabingwa wa Afrika nchini, klabu ya Cairo ilisema kupitia taarifa yake rasmi. 

Huu ni msimu wake wa pili akiwa na Zamalek, ambaye alijiunga nayo akitokea kwa mahasimu wao Al Ahly mwaka jana.
Hassan anatambuliwa na shirikisho la soka la kimataifa FIFA kuwa ndio mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi za kimataifa, akiwa ameiwakilisha Misri mara 184 kuanzia 1995 mpaka 2012. 

Hassan, ambaye ana rekodi ya kushinda kombe la mataifa huru ya Afrika mara nne, lakini hajawahi kucheza kwenye michuano ya kombe la dunia, pia aliwahi kucheza soka nje ya nchi katika klabu ya Anderlecht ya Belgium na Besiktas iya Uturuki.

No comments:

Post a Comment