Uongozi wa matawi wa klabu ya Yanga (wenyeviti na makatibu) leo
umefanya kikao katika makao makuu ya klabu mtaa wa twiga/jangwani kisha
kutoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamko la uongozi
(kamati ya utendaji) kutokubali kuonyeshwa kwa michezo yake kwenye
luninga.
Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano
na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na
kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya
kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake.
Akiongea na
waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema
baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es
salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na
viongozi juu ya haki ya matangazo.
Mmoja wa viongozi wa matawi
Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF
inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya
kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga.
Makele amesema
taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi
Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo,
haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani
kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo.
Kikubwa tunamuomba
rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani
mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi
bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki).
Huwezi
kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao
binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza
kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa
washabiki 8,000 kwa kila mchezo.
Mwisho
Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega,
tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote
wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu
pasipo kujibu hoja.
kinacho nichekesha Simba sc baada ya kuvita zile cheque za simba Tv hili wanaona kama aliwahusu.....hawa watu ni wanafki saana.BIG UP Dar young Africans A.K.A " Nyuma mwiko Daima mbele"
ReplyDeleteteteh kweli mike ni mbulula,hivi kweli washabiki wa tz wabinafsi sana,kwa vile hiyo pesa wanapewa wote ingekuwa yanga mngekuwa wa kwanza,mnaoji vi2 ambavyo avina mantiki,mbona mechi zenu zimeonyeshwa bure na susper sport amkulalamika kwavile kampuni ya nje
DeleteMdau lamadi simiyu
kama hiyo azam TV haijaanza kuonesha na hatujui iko wapi YANGA wanayo sababu ya kuhoji. isije ikawa Richmond katika soka. pili, sikubaliani na hoja ya Mwenyekiti wa Yanga kwamba mashabiki kutoenda uwanjani kutazinyima klabu mapato. ikiwa udhamini utakuwa unatija isitoshe watanzania tunapenda mpira. ikiwa ni mpenzi wa yanga kweli itakuwa vigumu kushindwa kwenda uwanjani kama timu yake inacheza. lIGI YA KENYA inamashabiki wachache sana wanaokwenda uwanjani lakini udhamini wa Supersport umevifanya vilabu kuwa afhadhali kifedha. na sasa ligi inaushindani. yanga wasigomee bali waangalie namna ya kulifanya hili liwe bora zaidi kwa ligi bora na timu bora. Mamea Kanumi. Moro.
ReplyDeletewe ujio makampuni ya azam?ila super sport inazijua,mpira majungu kwa vile azam ni kampuni ya tz
DeleteNenda shule kwanza,hautokuwa na hoja za kimbulula
Bigup sana yanga wajibu hoja zenu ndio cha msingi
ReplyDeleteMashabiki wa Yanga na viongozi wote ni wabinafsi
ReplyDelete