Search This Blog

Friday, August 2, 2013

BASKETBALL ALL STARS BONANZA:

BASKETBALL ALL STARS BONANZA:

 
Kama wasemavyo watoto wa Mjini kuwa Habari YA MUJINI  kwa sasa Ni Bonanza la mastar wote wa mpira wa Kikapu Dar es salaam na Tanzania kwa Ujumla.Vijana basketball Club imeandaa bonanza maalumu la mchezo wa Kikapu litakalo shirikisha wachezaji mbali mbali kutoka pande za jiji la Dar es salaam .Bonanza Hilo Litakalofanyika jumamosi hii(August 3) katika viwanja vya LEADERS CLUB KINONDONI ,kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa Kumi na Moja jioni.Litashirikisha Wachezaji wakali (mastar) katika mpira wa kikapu kwa ngazi Tofauti.Kutakuwa na Timu mbili pinzani katika kila Ngazi.Ngazi ya Kwanza Itakuwa ni ya VIJANA WADOGO(watoto) ambao watatengezeza timu mbili zitakazo chuana kuonyesha Hazina ya mpira wa kikapu kwa Miaka ya Baadae.Ngazi ya pili itakuwa ni ya wechazaji wakali(Bora) wa basketball wenye jinsi ya Kike(wanawake),ambao nao watafanya yao mapema kabla ya ngazi ya Tatu ya wakongwe wa Zamani Kuchukua uwanja.Wakongwe hao(VETERANS) nao wataonyeshana Ubavu kukumbushia enzi zao na kuonyesha ramani kwa chipukizi jinsi kikapu cha zamani kilivyokuwa.Katika kile kinachoaminika kusubiriwa na wengi Mjini,ni pale VIJANA waliopevuka,wakali na wanaosifika Tanzania Kwa mchezo wa Kikapu watakapo funga pazia la bonanza hili linalosubiriwa na wengi jijini Dar es salaam.
Bonanza hili litasindikizwa na Burudani Mbali mbali zikiwemo Element za HIP HOP (DJ,DANCING(B-BOY),FREE STYLE),Haitaishia Hapo watakao bahatika kufika watashuhudia burudani kutoka wasanii mbali mbali wa mziki wa Kizazi kipya na stand up comedies wakifanya yao kuongeza Radha.Wakishirikiana na mabingwa wa Burudani Tanzania CLOUDS ENTERTAINMENT watasimamia mpango mzima wa Burudani na mziki mzito eneo la Tukio.
Pia bonanza hili litapambwa na mashindano ya mchezaji mmoja mmoja katika vipengele Tofauti.Kutakuwa na mashindano ya kumtafuta mkali wa Kupiga DUNK,(slam dunk contests),mkali wa 3 points(3 points shoot outs),na mengine mengi ya ziada yatakayo fanywa kama Suprize.
Kiingilio katika Bonanza hili itakuwa ni shilingi elf kumi(10,000) tu kwa wakubwa na elfu tano(5,000) kwa watoto.Burudani na michezo weekend hii ni katika Bonanza la mpira wa Kikapu pale Viwanja vya leaders club.
  • OMBI KUTOKA KWA KATIBU WA VIJANA BASKETBALL CLUB wale wote wanaohitaji kushiriki kama wachezaji katika Bonanza hili, wanatakiwa wafike kuanzia saa nne mpaka saa tano kamili asubuhi kwa ajili ya kujiandikisha.
RATIBA KAMILI YA BASKETBALL ALL STARS BONANZA:

No comments:

Post a Comment