Search This Blog

Friday, August 2, 2013

LIGI KUU YA SIERRA LEONE - VILABU VYAGOMA KUCHEZA MPAKA MSHAMBULIAJI WA SIERRA LEONE ARUDISHWE KUGOMBEA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA CHAMA CHA SOKA CHA NCHI HIYO


Ligi kuu ya Sierra Leone imesimamishwa kwa muda usiojulikana kufuatiwa azimio lilosainiwa na vilabu 10 kati ya 14 vinavyoshiriki ligi kuamua kususiwa ligi hiyo jumatatu iliyopita.
Vilabu vilivyosusiwa ligi ni Diamond Stars, Gem Stars, Kambui Eagles, Old Edwardians FC, FC Kallon, Bo Rangers, Ports Authority FC, Mighty Blackpool, Central Parade FC, na Freetown City FC.
Vilabu hivyo vilichukua uamuzi huo katika kupinga kuondolewa kwa Mohamed Kallon na wagombea wengine wa uongozi katika uchaguzi mkuu wa chama cha soka Sierra Leone Football Association (SLFA), ambao utafanyika jijini Freetown siku ya jumamosi.
Meseji iliyotumwa kwenye vyombo vya habari badi inayoendesha ligi ilisomeka: "Katika kuamini usawa na kwa hatma ya mchezo tumeamua kuwasiliana na na mwenyekiti wa kamati ya haki na sheria ya SLFA baada ya kupokea barua iliyosainiwa na vilabu 10 vikielezea uamuzi wao wa kususa kushiriki kwenye ligi.  
"Wote - kamati ya ligi na SLFA wameamua kwa haraka kusimamisha ligi inayoendelea mpaka uamuzi mwingine utakapochukuliwa wakati mazungumzo ya utatuzi wa suala ukiendelea."
Mchezaji wa zamani wa Inter Milan na AS Monaco Mohamed Kallon aliondolewa katika kinyang'anyiro cha kugombea uraisi zikitolewa sababu kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo hajakidhi vigezo vya andiko la 32 (4) la katiba ya SLFA.
Andiko hilo linasema: "Wanachama wa kamati kuu wote ni lazima wawe raia wa Sierra Leone na inabidi wawe wameishi Sierra Leone kwa kipindi kisichopungua miaka mitano ili waweze kuwa halali kugombea nafasi ya kuchaguliwa."
Lakini, Kallon alikataa kukubaliana na uamuzi hupo, akisisitiza ni uamuzi wa kisiasa uliopelekea jina lake kukatwa .
Wagombea wengine wawili waliondolewa kwenye uchaguzi wa uraisi ni Rodney Michael na Foday Turay, wote kwa sababu wote wapo kinyume na andiko la 25 za maadili ya FIFA ambalo linadili na uchezaji wa kamari na mambo mengine yanayohusiana na kamari kwenye mchezo wa soka. 
Lakini wakati huo huo, Raisi wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ameingilia kati suala hilo na anajaribu kulitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Mashabiki wanaomsapoti Kallon walifanya maandamano ya amani mbele ya ikulu ya nchi siku ya Jumatatu kuelezea kutoridhiswa kwao na uamuzi wa kuondowa wagombea kwenye uchaguzi isivyo sahihi. Mpaka sasa Raisi 
Koroma ameshafanya mikutano miwili na viongozi wa SLFA na wagombea walioenguliwa, wakati huo waziri wa michezo wa nchi hiyo kwa pamoja na wagombea, SLFA na FIFA watafanya mkutano wa mwisho wa pamoja siku ya leo. 
.
Mpaka sasa kwenye uchaguzi huo amebakia mgombea mmoja tu kwenye nafasi ya uraisi Isha Johansen na kama mambo yataendelea kama yalivyo basi mwanamke huyo atapita bila kupingwa.

1 comment: