Search This Blog

Friday, August 2, 2013

SAKATA LA GARETH BALE; TOTTENHAM INAPASWA KUMUUZA BALE ILI KUWA TIMU IMARA ZAIDI

Ikiwa umekaa sana kwenye dunia ya biashara, kuna kundi la maneno mawili lazima uyazoee: "Fedha ni nguvu" na "kila mtu ana bei yake."  Barclays Premier League ni biashara kubwa sana, hasa kwa vilabu vikubwa vya juu, mahala ambapo Tottenham inapataka kwa hali na mali - kuwa miongoni mwa vilabu vinne vya juu na kujijengea uhakika wa kucheza champions league kila mwaka. Baada ya msimu miwili kuikosa michuano hiyo kwa pointi chache tu, sasa swali ni namna gani wanaweza kutimiza lengo, na huku Real Madrid wakiripotiwa kumtaka Gareth Bale, Tottenham sasa wanaanza kuona nguvu ya maneno ya "Fedha ni nguvu" na "kila mtu ana bei yake." 

Kama taarifa za vyombo vya habari ni zakuaminika, Real Madrid wapo tayari kuvunja rekodi ya muda wote ya uhamisho ili kumpata Bale, kwa kulipa kiasi cha £86 million ($135 million U.S.). Bei hiyo ni zaidi paundi millioni 6 zaidi ya zile alizonunuliwa Cristiano Ronaldo mwaka 2009 akiwa na miaka 24 kama ilivyo kwa Bale sasa.

Kwa vyovyote vila ambavyo Bale alivyokuwa kwenye kiwango kikubwa, na kuwa na msaada mkubwa kwa Spurs kiasi cha kukaribia kuiondoa Arsenal kwenye Top 4, lakini Bale hajafikia kiwango cha Ronaldo wakati akinunuliwa na Madrid, na kwa hakika sio mchezaji mwenye kiwango kikubwa mara tatu zaidi ya wachezaji wengine wa EPL.  Kuna ubishi wenye maana umetengenezwa kwamba Luis Suarez ni mchezaji mzuri aliyekamilka kuliko Bale kwa sasa, na bei yake inaweza kuwa kuanzia 30-40 million pounds ikiwa atauzwa kwenda Arsenal akitokea Liverpool.

Hii ni kama kusema kwamba: Hakuna namna ambayo unaweza kusema Gareth Bale ana thamani kubwa kama inavyotajwa, lakini pamoja na yote haya, sioni sababu kwanini Spurs wasimuuze kijana huyu.

Kama Spurs watang'ang'ania kubaki na Bale White Hart Lane utakuwa ni uamuzi ambao umetokana na kujijenga kuwa klabu yenye wachezaji wakubwa - ambapo klabu inayojitutumua kama Tottenham haitaki kupewa jina la 'muuzaji' kwa klabu tajiri. Madrid tayari ilishamnyakua Luka Modric kutoka Spurs msimu uliopita, na inaonekana ndivyo itakavyokuwa siku kadhaa zijazo kwa Gareth Bale.
Katika cheni ya chakula ambayo ndio hatua ya juu ya soka barani ulaya, kama hauli, then unaliwa, na hii ndio hali ilivyo kwa sakata la uhamisho wa Bale baada ya Modric kuchukuliwa kwa Spurs bila wao kupenda kutokana na misuli ya kifedha ya Madrid.

Mashabiki wa Spurs wana haki kuamini wana timu yenye nguvu ya kutosha kuweza kuingia kwenye top 4 ikiwa wataweza kumbakiza Bale. Klabu ilimaliza nafasi ya nne misimu miwili iliyopita (huku Bale akiwa hana kiwango alichokuwa nacho msimu uliopita), lakini walinyimwa nafasi yao ya kushiriki Champions League baada ya Chelsea kushinda ubingwa huo wakati wakiwa wamekosa nafasi kwenye ligi - wakimaliza nafasi ya sita. 


Msimu uliopita, Tottenham walimaliza pointi moja nyuma ya mahasimu wao Arsenal. Ukiwaongeza wachezaji wapya Paulinho na Nacer Chadli kwa pamoja Soldado, then kuna sababu nzuri ya kuamini kwamba Spurs wana timu nzuri kufanikisha ndoto yao wakiendelea kuwa na Bale.

Lakini itakuwa jambo la maana kiuchumi kumbakiza Bale? Sawa, watashika nafasi ya nne kwenye ligi (na labda wataingia kwenye hatuya ya makundi ya Champions League ikiwa watashinda kwenye mechi za awali) then watakuwa wameingiza kiasi cha chini sana £13 million kupitia mapato ya haki za matangazo ya TV na bonasi, na kiwango hico kinaweza kuongezeka kutokea hapo. 
Mara ya mwisho Tottenham kucheza Champions League msimu wa  2010-11, klabu iliingiza kiasi cha millioni £27, baada ya kucheza mpaka robo fainali na kutokana na mapato ya haki za matangazo ya TV. Wakati Manchester United ilipofungwa na Barcelona katika fainali msimu huo huo, klabu hiyo ilitengeneza kiasi cha £45million, ukiangalia na kiasi walichoingiza mwaka mmoja kabla waliposhika nafasi ya katika ligi kupitia mapato ya TV ya mechi za Premier League. Hivyo ukifananisha na walichopata kwenye Uefa Champions League unakuja kugundua vilabu vya England vinatengeneza fedha nyingi kwenye EPL kuliko barani ulaya.

Hivyo, kwa misingi ya kibiashara iliyopo, ikiwa Danie Levy (mwenyekiti wa Spurs) na wenzie, wakiweza kumbakiza then wanaweza kucheza Champions League msimu wa 2014-15, na kwa kufanikisha hilo litawasogeza juu kwenye msimamo wa EPL hivyo kuweza kujihakikishia ushiriki wa michuano ya ulaya - hivyo wakiingiza fedha nyingi zaidi za matangazo ya TV na bonasi kutoka kwenye UCL na EPL, kwa jambo hili unaweza kutetea uamuzi wa Spurs kutaka kumbakiza Bale angalau kwa msimu mmoja. Akiepukana na majeruhi, atakuwa kwenye kiwango kilichoimarika zaidi na thamani yake itakuwa juu sana, hata kama Madrid hawatokuwa tayari kulipa fedha nyingi kumsajili. Lakini hili litawezekana ikiwa kama Bale atakuwa sawa kisaikolojia baada ya kufeli kwa uhamisho huu - na kuweza ubora ule ule aliokuwa nao msimu uliopita uwanjani, jambo ambalo ni kama kucheza kamari - ukizingatia mchezaji mwenyewe amesharipotiwa kwamba anataka kuondoka Spurs na ameshamwambia kocha wake kwamba akili ipo Madrid. Huu ni ushahidi tosha mchezaji anaweza akavurugwa kiakili ni jambi hili la usajili kama halitoenda kama nafsi yake inavyotaka.

Ndio, japokuwa kuna uwezekano wa Spurs kufuzu kucheza Champions League, lakini kukataa kiasi cha £85 million ni ujinga ukiangalia na thamani halisi ya mchezaji, tena kama habari za vyombo ni za kuaminika kwenye dili hilo bado Spurs watapewa na Angel Di Maria - utakuwa ni ujinga kukataa ofa ya namna hiyo. Kwenye hiyo Millioni 85 wanaweza wakalipia uhamisho wa Soldado kwa £25m, pia wanaweza wakamsajili mchezaji mwingine mwenye thamani ya £30m na bado wakabikia na chenji ambayo wanaweza wakanunua wachezaji wengine kadhaa kukiongezea uimara kikosi chao.

Chadli ni mchezaji mzuri sana ambaye anaweza akaleta ubora mwingine kwenye kikosi, aliigharimu Spurs £7 million.
Ukiangalia kikosi cha sasa Spurs, hakuna ubishi wa maana unaoweza kuuleta kwa kusema kwamba Di Maria, Soldado, Lennon, na mtu Julian Draxler wa Schalke itakuwa sio timu nzuri kama akiwemo Bale pekee yake.
Watu wengi wanakisia kwamba kuuzwa kwa Bale hivi sasa kutakuwa sawa na Spurs kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi za kucheza Champions League, wakati kuuzwa kwa Bale kutawapa uwezo Spurs kutengeneza timu nzuri zaidi kwa fedha nyingi watakazopata.

Kwa vyovyote itakavyokuwa Spurs hawawezi kupata dili zuri zaidi hili ambalo Madrid wanaripotiwa kutoa, kuendelea kukaa na Bale na kamari, anaweza akaisaidia timu au akashindwa. Fikiria akiumia na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu Spurs watakuwa kwenye hali gani? Maoni yangu ni bora auzwe - ili timu isijengwe kumtegemea yeye tu - auzwe timu ipate fedha nyingi za kuweza kutengeneza kikosi bora na cha ushindani kuliko cha sasa.

No comments:

Post a Comment