Search This Blog

Thursday, December 6, 2012

MJADALA: NINI MAONI YAKO JUU YA HILI SAKATA LA KUUZWA MRISHO NGASA!

38 comments:

  1. Hivi mchezaji akipelekwa club nyingine kwa mkopo wa mwaka mmoja (kama Ngasa), klabu ya awaali inaweza kumchukulia maamuzi yoyote akiwa ndani ya klabu ya mkopo kama kumuuza, kumrudisha ktk timu ya awali au kumchukulia hatua za kinidhamu kabla ya muda wa mkopo kumalizika?
    Hivi TFF hawana nakala za mikataba ya wachezaji na klabu zao?

    Emma

    ReplyDelete
  2. kaka mimi ni mpenzi sana wa mpira wa miguu na klabu yangu ya Simba, kabla ya yote mimi nimecheza na Ngassa Mza, katika klabu moja hivi ya pale magomeni ilikuwa ikiitwa Crisk Mwanza chini ya Mwl J. Mimi ni mdada lkn. kaka maisha yanasafari ndefu sana kiaci kwamba tunapitia milima mirefu, mipando na miteremko pia bila kusahau utelezi katika maisha. swala la Ngassa kwa Sudan ni habari ya maisha maana kwetu tunasema MPIRA PESA, sasa aachwe aende kijana anatafuta maisha na si maisha yamtafute yeye. Kipaji kimeonekana Nyota imeng'ara bidii imeoneka,chamsingi tuuage kwa amani na tumtakie kila la kheri aendako kuwe salama ila achunge sana kiwango chake kisishuke, akaongeze bidii zaidi ila tu awe makini na nidham yake huku akiangallia sifa ya nchi yake na mzazi wake, Binafsi ninaunda sana uchezaji wa Ngassa ila tu ajitahidi sana kuongeza stamina maana kama vile sio saaaaaaaaana pale kwenye stamina. KILA LA KHERI SAFISHA NJIA NA WENZAKO WAONE MWEZI KILA LENYE FANAKA LIWE NAWE, AMINA.

    ReplyDelete
  3. Mr. Malangahe JosephDecember 6, 2012 at 9:54 AM

    Azam, Simba wote wa makosa.
    Maana yake ni nini, Ngassa alienda Simba kwa mkopo na ada ya mkopo ni 25m kama ulivyo utaratibu, hivyo Ngassa ni mali ya Azam kisheria pia Azam hawezi kufanya chochote juu Ngassa kwa kuwa muda wa mkataba haujaisha na kama mkataba umeisha Azam wanahaki ya kumuuza Ngassa popote ulimwenguni. Hivyo Azm na Simba wakae mezani/chini wazungumze, kama mkataba haujaisha na Ngassa anahitajika ni jukumu la Azam kuununua mkataba wake kwa kurudisha baadhi ya gharama ili Klabu mama (Azam) iwe huru kumtumia ionavyo. Zaidi ya hapo ni ubabaishaji wa viongozi wetu wa soka nchini. Issue ya Ngassa mfano wake ni kama wa Tevez kwenda Man U kutoka Westham huku akimilikiwa na kampuni nyingine.

    ReplyDelete
  4. viongozi wa simba wamezidi kuwa wazembe sana. mchezaji umemchukua kwa mkopo toka azam ambaye alibakisha mwaka moja katika mkataba wake kwa hiyo ilitakiwa simba waongee na azam kuwa pamoja na kumchukua kwa mkopo mchezaji pia wamchukue jumla kwa hiyo wangemalizana na azamlakini viongozi wanajifanya wanajua sheria za soka kumbe wazembe. halafu wanailaumu tff eti inawahujumu hiyo kitu ipo wazi kabisa. AZAM WANA RIGHTS ZOTE ZA KUMUUZA NGASSA KWA EL MERREIKH YA SUDAN NA YANGA WANASUBIRI MGAWO WAO WA 5% PAMOJA NA KAGERA SUGAR PIA 5% YAO KIULAINI. SIMBA IMEKULA KWAO WAKAJIFUNZE SHERIA ZA USAJILI BADO OKWI NAYE ANATAKIWA NA AL HILAL YA MISRI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeuona mkataba kati ya azam na simba? na simba na ngasa? au kwa sababu unajua akina mgongolwa wataendelea kutafsiri tu zile kanuni zao wanavyojua

      Delete
    2. Hivi ukikaa kimya utaonekana hujui mpira? maana hapa umejianika mtu mzima...weka mkataba wa simba na Azam na Simba na Ngasa vinginevyo funga domo lako...
      Yegella

      Delete
  5. shafih tusaidie kujua yeye kama muhusika mkuu,amekubaliana na hili swala,nakumbuka mwenyewe alishaongelea swala la kucheza south africa,hili swala la kucheza sudan mwenyewe analizungumziaje

    ReplyDelete
  6. Wote Azam na Simba wana makosa.
    Azam hata kama alikuwa ana mkataba unaomruhusu kumrejesha mchezaji katikati ya kipindi cha mkopo (ambayo sidhani kama sheria za mpira Tanzania zinaruhusu) lazima alitakiwa kuwajulisha walie na mchezaji kwa sasa maana kuna masuala ya makabidhiano ya vifaa vya klabu na mali nyingine. Ila pia Simba wana makosa ya kuingia mkataba juu ya mkataba na Azam bila kuwajulisha Azam officially--hilo nalo ni kosa ingawa kiuharisia kwa kuwa Ngasa alikuwa amebakiza mwaka mmoja na huo huo ndio kipindi cha makubaliano ya mkopo ina maana immediately after mkopo alikuwa huru hivyo kimantiki unaweza kuingia mkataba kama hakuna kipengele cha kurecall back-practically no!
    Azam wanajua walifanya makosa ndio maana inawezekana wametangaza pesa kidogo ya mauzo ili kama kutatokea kuamuliwa kugawana wagawane walichotangaza the rest ambacho hawakutangaza chao.
    Tatu Ngasa nae ana makosa maana anajua ana mkataba na simba kwa nini asaign mwingine bila kuwajulisha----haya yote yanaletwa na uongozi dhaifu wa TFF kwa kufumbia foul zilizochezwa kwa Yondani na Mbuyi Twite. Ila pia tunakoelekea timu zitaacha kuruhusu wachezaji waende kambi ya Taifa maana hakuna usalama kwa wachezaji tena.
    kuna mengi ila tusijaribu kufananisha sana mikataba ya Ulaya na hapa ambapo hata kanuni za TFF zenyewe hazina tafsiri inayoeleweka.

    ReplyDelete
  7. Simba na Azam ndio wanajua ukweli wa hili,tuache kuingiza siasa kwenye ueledi,mtu pekee wa kumfunga paka kengele ni Ngassa nwenyewe,km aliweza kusimama na kusema ukweli ktk sakata lake na azam hadi akapelekwa simba,basi naamini hata hili pia ataweza kusimama imara na kusema ukweli kwa faida yake na taifa kwa ujumla,Ngassa ndiye atakaye tegua kitendawili hiki..

    ReplyDelete
  8. Baada ya majadiliano ya Simba na Azam, tunaomba Ngassa aachiwe na aanze maisha mapya Sudan, sehemu ambayo hatakuwa na washkaji wanaokula muda wake mwingi, sehemu ambayo haitakuwa rahisi kwake kuchukua chukua mademu tu, sehemu ambayo hatakuwa free kulakula bata hovyo na hivyo ku settle mind yake na kufocus kwenye mazoezi na kazi yake kwa ujumla, hapo ndipo tunaweza kuona matunda yake baada ya kipaji kuunganishwa na juhudi (mazoezi)......... ALL THE BEST BRAAH

    ReplyDelete
  9. Kwangu nashindwa kuwalaumu azam coz hakuna asiyejua kuwa Ngassa ni mali halali ya Azam na SIMBA yupo kwa mkopo wa thamani ya Tsh 25mil so swala Azam kumuuza inategemea na vipengele vya mkataba baina ya AZAM na SIMBA bt kwa faida ya mchezaji na soka la Bongo tumuache kijana aende Sudani!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu kwenye kanuni hakuna mambo ya tumuache kijana akapate maisha. Tatizo wote hatujauona mkataba wa azam na simba na simba na ngasa, ila tunachojua na kiko wazi ni kuwa ulikuwa ni mkopo wa mwaka na sidhani kama Tanzania kwa kanuni za TFF unaweza kumrejesha in between unless mkataba unasema wanaweza kumuuza---na je ni bila kumuuliza anayemmiliki kwa sasa. Twende mbele twende nyuma TFF ndio kiini cha haya matatizo kwa kufumbia macho yaliyotendeka nyuma--wameshatengeneza reference(yaleyale ya Twite alikwenda APR kwa mkopo muda wake wa mkopo ukaisha wakampa mkataba mpya---yanga akaenda akakuta pale APR wameshamuuza mchezaji wao wakawadokeza kuwa originally walimchukua kwa mkopo then ikawa loophole--the same approach imetumiwa na elmereikh walipona simba pagumu wakatumia the approach wakijua kuna reference case iliyobarikiwa na TFF then Mungu akupe nini?
      TFF waweke katiba na kanuni kwenye website yao wote tuzione na kuzijua (na vioja vitaendelea sana)

      Delete
  10. Vip sasa Gari atarudisha na zile milioni 25? Mkataba wake na Simba ni batili maana kulingana na FIFA regulations mchezaji anaweza kusign na timu nyingine 6 months kabla ya mkataba wake kuisha. Sasa kama mkataba wa Ngasa unaisha June 2013 mkataba wowote wa Simba kabla ya January 2013 ni BATILI...
    Ila Pia makubaliano ya Simba na Azam yalikuaje maana huwezi mpa mtu mkopo halafu uje ghafla umnyang'anye.. Nionavyo mimi lazima kuwe na compansation....

    ReplyDelete
  11. Kwa upande wangu naona Azam wamefanya jambo la maana kwa kumuuza Ngasa ila vipi kuhusu Simba kwasababu alikuwa ana mkataba wa mwaka mmoja kwa mkopo ila na mshahara alikuwa anapokea kutoka kwa Simba sasa hapo maana ya mkopo nnini kaka Shaffih watawarudishia Simba pesa zao au la hapo kidogo sipaelewi tusubirie uamuzi utakao tolewa baina ya hizo timu mbili ila kwa Ngasa kwenda nje nchi it's good jamani tuache siasa kwenye mpira ngoja vijana wetu wakajaribu akishindwa atarudi hayao ndio ya kwangu God bless Ngasa God bless Tanzania by Kamongo

    ReplyDelete
  12. Kwa mtizamo ni kwamba Azam ndio wa miliki halali wa Ngasa na hatujui terms za ukopeshaji katika mkataba baina ya azam na simba zilikuaje..Inavyoenekana Azam wanahaki ya kumrudisha Ngasa wakati wowote wanapomhitaji akiwa simba na pia Simba hawana mamlaka ya kumuuza Ngasa popote..Elmerekh hawakuwa wajinga pia kujadiliana na Azam badala ya Simba..Hivyo kama kuna mikataba zaidi iliyotokea kati ya Simba na Mchezaji Ngasa kuliko ule wa Simba na Azam then huo ni uzumbukuku wa Simba wenyewe kuvuruga mambo na hapa TFF wanapaswa kuwawajibisha Simba..Ila Ngasa ni mali ya Azam iliyokua Simba..Azam wanahaki kumuuza Ngasa, maana mikataba mingi ya ukopeshaji ni kwamba mwenye haki zote za mchezaji ni timu inayokopesha na sio inayokopeshwa

    ReplyDelete
  13. Hivi inakuwaje mchezaji anapelekwa kwa mkopo club X kwa mwaka m1 ambapo anamkataba wa mwaka m1 tu na club y baada ya hapo mchezaji huyo atakuwa huru. Club X inaamua kumsainisha ikiwa na maana kuwa akimaliza mkataba wake na Club Y atakuwa mchezaji halali wa Club X. But ghafla club Y inaamua kuvunja mkataba wa wa mchezaji huyo na kumuuza klabu Z. Kwel soka la bongo uchafu mtupu.
    Mchezaji yuko kwa mkopo club fulani iweje klabu hyo ikikutana na klab mama yake anacheza mach hyo?

    ReplyDelete
  14. Kimantiki, sidhani kama klabu inaweza kuwa na maamuzi kwa mchezaji aliyetolewa kwa mkopo katikati ya msimu bila waliomchukua kuhusishwa. Kama ingekuwa hivyo basi wangeweza hata kumwambia asicheze mechi na ikiwa hivyo timu iliyomchukua ina control gani na mchezaji?Suala la pili, kama mkopo ulisema ni kwa mwaka mmoja ambao bado haujaisha, kulikuwa na maana gani kuongelea muda katika mkataba? Sitaona ajabu maamuzi yakatoka bila maswali ya msingi kujibiwa maana kwa viongozi wa soka waliopo Tanzania lolote linawezekana inategemea nani wanaokaa ktk kamati kutafsiri kanuni na taratibu.

    ReplyDelete
  15. Mosi ni kuwa Azam hata kama wasingekuwa wamelipwa pesa na Simba walitakiwa kuwajulisha Simba kuhusu hilo kwa sababu mkataba ni wa mkopo wa mwaka mmoja na sidhani kama ulikuwa na kipengele cha kumchukua muda wowote hapo katikati kabla ya mwaka mmoja kumalizika.Na hata kama kingekuwepo, taarifa ilikuwa muhimu kabla ya hayo maamuzi. Hata kama ni mkopo, bado unaitwa MKATABA.
    Ikiwa hilo limeshatokea, Azam bila shaka itakuwa imekiuka makubaliano na kwa vyovyote hawawezi kukwepa hilo.
    Simba hatuna sababu ya kusema ule haukuwa mkopo kwa sababu tulilipa hela, mikopo ya hela ipo, Kimsingi ni kung'ang'ania Azam(walilipwa mil 25) na Ngassa (alilipwa gari, mil 12 ili atumike miaka miwili sio miezi michache tu) watucompensate gharama zilizotumika kwa sababu mkataba (haijalishi wa mkopo au mauzo) umekatishwa kabla ya mwaka.
    La mwisho naweza kusema Viongozi wa mpira tubadilike, mambo bado yanafanyika kiholela sana, si wa Azam, si wa Simba, Si wa Yanga.

    ReplyDelete
  16. VIONGOZI WA SIMBA WANAFANYA BIASHARA MIKATABA WANAYOINGIA NA WACHEZAJI WANATENGENEZA VIPENGELE DHAIFU KWA MAKUSUDI ILI WAWEZE KUMUUZA MCHEZAJI HUSIKA KWA KUTUMIA VIPENGELE HIVYO, HAIINGII AKILINI HATA KIDOGO RAGE KAMA MWANASHERIA AU EVODIUOUS MTAWALA AMBAYE NI MWANASHERIA NA WENGINE WENGI WAKUBALI TU KIRAHISI RAHISI KUKUBALI MCHEZAJI AEND TIMU NYINGINE NA AKIWA NA MKATABA ULIO HALALI HII WANATUPIGA CHANGA LA MACHO SISI WANACHAMA NA MASHABIKI, HII NI BIASHARA BANAAAA!!!!!! HAINA UBISHI.

    ReplyDelete
  17. Rage maneno mengi utekelezaji hakuna, mpira sio siasa aache kukurupuka bana, ukweli ni kuwa ngasa ni Mali ya azam. Wanayo haki ya kumuuza.

    ReplyDelete
  18. Kama kwenye mkataba wa mkopo kuna kipengele kinaruhusu haya.. hakuna shida. ila kwa maono yangu kwa kuwa ngasa muda aliokuwa amebakiza na AZAM wamempeleka SIMBA. Ina maana AZAM wamebugi meen.

    ReplyDelete
  19. ni haki kwa azam kumuuza ngasa wanachotakiwa ni kurudisha nusu ya hela ya simba coz tayari simba wamemtumia kwa nusu ya mzunguko wa kwanza. kuhusu simba na ngasa kupeana gari na m12 ni makubaliano ya ngasa na simba tuwaachie wenyewe

    ReplyDelete
  20. Watu wengi wamechanganya ile 25m simba waliyolipa azam. Wanafikiri ni transfer fee. Mzee rage jana mapovu yalikuwa yanamtoka Clouds. I think ile ni LOAN FEE! Walipokosana naye, sakata la kukiss logo Ya Yanga,Bei yake Azam walitangaza ilikuwa 64m (minimum USD 50,000). Simba wakawa na 25m, Yanga 20m. Nadhani 25m ilikubaliwa kama LOAN FEE, mshahara wamlipe yani 2m kila mwezi! mpaka mkataba wake na Azam utakapoisha! Wenye mchezaji ni Azam na wana uhuru wa kumuuza, ili mradi mchezaji akubali kwenda timu mpya na ajadili maslahi yake na timu mpya. Kule (El Merreikh) atapata kama 4,000 USD kwa mwezi, gari, nyumba, posho, bonus etc. Kwa muono wangu mdogo habari ndio hiyo jamani!

    Kwa upande mwingine, Simba wangeweza kunegotiate aslimia ya share yao iwapo mchezaji atauzwa timu nyingine. Nadhani hawakufanya ivyo, kwa iyo 100% pesa itaenda Azam

    ReplyDelete
  21. mimi sio mtaalam sana, ila naomba nifahamishwe kitu kimoja tu, mchezaji anapotolewa kwa mkopo kwenda timu nyengine halafu zinakutana zile timu mbili iliyomtoa na iliyomchukua kwa wakate ule je anaruhusiwa kucheza, au kulikua na makubaliano kati ya simba na azam? maana ngassa alicheza siku ya simba na azam

    ReplyDelete
  22. Simba arudishiwe gharama zake tsh m 25 na marupurupu kidogo waliyomgharamia ngassa kwa muda wote alokuwapo simba then wamwache kijana akapge soka huko sudan huenda huu ndio mlango wa yeye kusonga mbele zaidi. all da best, nitakukumbuka sana mtoto wetu wa jangwani.

    ReplyDelete
  23. Viongozi wetu hawako makini.
    Jana na leo nimemsikiliza Mh Rage, kwa umakini na, ni kama wao (simba) waliwatega Azam kwamba kwa kulipa milion 25, basi mkataba ni wa mkopo. Mh Rage aliulizwa swali ambalo hakulijibu moja kwa moja.
    Maestro: "..mkataba una neno mkopo..."
    Mh Rage: "...hata kama lingekuwepo.." mwisho wa kunukuuu. Hii ina maana mkataba una sema wazi (explicit) kwamba ni mkopo. Kwa nini Mh Rage anataka kuufanya uwe "implied" total transfer?. Nashukuru mazungumzo ya jana ya Sports xtra, Shafii na Geff walitoa mifano mbali mbali, ambayo km hili swala litaenda mbele mifano hiyo ni "precedent" tosha. Kwa hili Azama wanaweza kupigwa faini. Hata wao (Azam) wameshajiandaa, maana nilimsikia Manager wao akisema wako Tayari kuwarudisha Simba milion 25 zao. Pia hawatadai chochote in respect ya simba kumtumia Ngassa kwa kipindi hicho cha miezi 6.

    Kwenye hili Mh Rage wala asipoteza rasilimali za klabu kuishtaki Azam. Wachukue 25 M waangalie ustaarab mwingine.

    Naomba kumuuliza Maestro hii mikataba ya wachezaji haijadiliwi kwenye kamati tendaji? Kwa nini kila mara inaonekana km Mkiti mtaalam? Maestro hakuwapa ushauri juu ya hili?

    ReplyDelete
  24. Hakuna hata siku moja Simba na Azam waliwahi kushindwana katika deals za soka la bongo.Hawa jamaa wanafahamiana, wana undugu, hubadilishana wachezaji,hukopeshana wachezaji.Huingia deals mbalimbali za kisoka.Wala mapuvu yasiwatoke mashabiki.Kwa hili wao wanajuana vizuri tu.

    ReplyDelete
  25. Mimi nawapongeza Simba kwani wanazidi kuonyesha kwamba wao ndio Gate la kutokea wachezaji.Mchezaji hapati kuitwa nje ya nchi kucheza soka la kulipwa hadi atoke Simba.Mfano Henry Joseph,Mrwanda,Boban,Samatta,Kisiga,Mgosi,owino na sasa Ngasa.
    Ngasa amehangaika sana akiwa Yanga,Azam ili akacheze kulipwa ilishindikana,ile kukanyaga Simba tu,hata nusu mwaka bado kitu na box.Nawapongeza Simba kwa hili na waendelee na hii mentality ya MPIRA PESA.
    Nina hakika Simba hawatamzuia Ngasa kwani ni moja ya malengo yao kuona wachezaji wanapata mafanikio

    ReplyDelete
  26. Kwa mara nyingine tunaona ubovu wa viongozi wa klabu zetu kushindwa kutafakari sheria na kanuni zinazoendesha mchezo wetu huu wa mpira wa miguu.
    Ngasa alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Simba kwa makubaliano ya mwaka mmoja.Mchezaji unapokuwa kwa mkopo na klabu hiyo mara nyingi klabu inayokuchukua inalipia either gharama zote na mchezaji ikiwepo mshahara na malazi au kiasi fulani kwa mahitaji ya mchezaji.Sheria za umiliki zinabaki kwa 100% kwa timu ilyomtoa kwa mkopo.

    Kwa upande a Azam kosa lao litakuwa na kumwuza kwa El Merreck bila kuwataarifu Simba kwani kipindi cha mkopo kilikuwa bado hakijaisha kama walivyokubaliana.Ingawa suala hilo linazungumzika.

    Sula la Simba kuingia mkataba na Ngassa baada ya mkopo kisha itakuwa magumashi tu ya simba kama walivyofanya kawa Yondani. mara nyingi Viongozi wa Simba wameonyesha kuwa mbumbumbu na sheria hizi ama kwa kutokujali au kwa umazoea au kwa ujanjaujanja tu. Kumbuka suala la Mbuyu Twite, Yondani na sasa Ngassa na baade kidogo Okwi.

    Nawataka sana wanachama wa klabu hizi kubwa waangalie viongozi wao wana ujan ja ujanja au kutokujua sheria zinazoendesha mchez\o huuu.

    ReplyDelete
  27. kuuzwa ka ngasa c tatizo,shida kauzwaje?kaka shaff mm ninachojua mtu kupelekwa kwa mkopo timu fulani kuna mambo ya mcngi huangaliwa ila mimi nitaongelea mshahara,ngasa analipwa mshahara na simba kila mwezi,lakini pia ngasa alipekwa simba kwa mkopo au aliuzwa?maana simba wamewapa azam 25m hz pesa zlikuwa za nn?mkopo ninao ujua mm ni NIPE NITAKURUDISHIA sasa hz 25m zilikuwa za nini???HAPA KUNA TATIZO PANDE ZOTE.

    ReplyDelete
  28. Kwa upande wangu mimi ninaona kama simba wamechemsha na sio hili tu.Tuseme ukweli simba ina wachezaji wachache sana au haina wachezaji kabisa:Kwa uelewa wangu simba ni kama group ya marafiki fulani wanaamua kununua wachezaji halafu wanawapeleka simba,na hii ndio maana wakitokea wamepata soko nje anayelipwa ni yule aliye mleta ananufaika japokuwa hawakuliweka wazi hili suala, kiasi kidogo sana simba inapata(ganji kuona)
    Ndio maana ukitokea ugomvi kwenye timu,kila mwenye mchezajia anamuamrisha mchezaji acheze chini ya kiwango,hata makocha ni hivyo hivyo.
    So kwa namna yoyote ile simba watapewa ganji kuona:
    Kuhusu Ngasa Mwenyewe mi si dhani kama anaweza kumudu maisha ya sudani:alafu namshauri kabla ya kusaini aende akaangalie ugumu wa maisha wanaweza wakampa $ 4000 kumbe wala sio kitu kwa gharama za kule:Pia Eli mereikh sidhani kama wataweza kum export,timu nzuri kwa kusaidia mchezaji auzwe ni pamoja na simba.
    Mwaka huu mwanzoni pia nilienda Rwanda maisha ni ghali sana na vyakula ni tofauti na huku.
    Ningependa aende South africa

    ReplyDelete
  29. kwa upande wangu niko tofauti kidogo,sijawahi sikia mchezaji amefanikiwa tokea sudan,hapa nina maana hata kama shida ni pesa kwa azam na ngassa ama simba ila sioni mafanikio kwa mchezaji kama atakwenda kucheza kwenye ligi dhaifu zaidi ya tanzania ndo maana timu zao kwenye kagame tu zinashindwa kufanya vizuri tofauti na michezo ya kimataifa ambayo hufanya vizuri kwa hila za waarabu,mi nadhani ngassa njia sahihi ni kuelekea south africa ambako kuna timu zinamtaka tofauti na hawa waarabu sioni kama itakuwa busara kwa ngassa kwenda huko,tuache ushabiki maandazi jamani kama kweli tunamtakia mema ngasa hebu tumshauri achague south africa na sio sudani,nani asiyejua kuwa hata ulaya huangalia ligi ya SPL nani anaangalia ligi ya sudan?ili iweje?umefika wakati hata hawa wachezaji wetu kuwa na akili ya kufikiria kwa nini nyionzima alikataa kwenda sudan???hakuna tofauti na tanzania na kama kigezo ni dolla elfu 50 hata ukicheza poa within a year anaweza kuzipata hapa hapa nyumbani tofauti na kwenda kuanza maisha mapya huko sudan huku usijue wanaishije yaani maisha ya huko yako vipi lazima tujiulize kwa nini wewe na sio nyionzima????????????????badilikeni ndugu zangu tutoe ushauri wa msingi kwa mchezaji husika na taifa,samatta alitakiwa na timu moja kubwa ulaya katumbi akamuuliza utamlipa kiasi gani jamaa kiasi alichotaja katumbi akaongeza milioni 4 juu ya mshahara wa samata,nini naweza kusema kwa ngassa ni kitu kimoja ''NGASSA KEEP ON HARD WORKING ONE DAY YOU WILL GET PAID FROM YA HARD WORK''
    asanteni hizo ndo pumba za JIWE MWANAKIJIJI

    ReplyDelete
  30. Kabla ya mkopo, Azam walikuwa na haki zote kummiliki Ngassa kwa mwaka mmoja tu, na Simba ingeweza kusubiri iongee na Ngassa bila ya ruhusa ya Azam.

    Ndani ya mkopo, Azam wanaweza kuvunja mkataba wa mkopo na Simba, lakini pia Simba wana haki ya kukataa kuvunjwa kwa mkataba hadi muda wa mkopo uishe.

    Baada ya mkopo wa mwaka mmoja kwa Simba, Ngassa vile vile atakuwa amemaliza mkataba na Azam, so kwa ufupi Azam hawana haki na mchezaji baada ya mkopo.

    Yote hayo yatateguliwa iwapo TFF itasema bayana kuwa Ngassa ana leseni ya kuichezea timu gani kwa sasa, in such a way that ikitokea ITC ikahitajika kutumwa, TFF wanajua maombi ya ITC yapelekwe kwa klabu gani. Maombi ya ITC ya El-Mereikh (kupitia chama chao cha soka)kwenda klabu ya Bongo (kupitia TFF)ndio yatakayotoa sura ya kuonyesha nani ni nani kuhusu umiliki wa Ngassa. TFF italazimika kuifuata klabu yenye leseni ya sasa ya Ngasa, so swali lipo hapo, ni Azam au Simba?

    Kwa ufupi TFF ndio wenye jibu kuhusiana na leseni anayotumia Ngassa kucheza ligi kuu ya Bongo. Nina wasiwasi kuwa El-Mereikh wameliwa bure fedha zao

    ReplyDelete
  31. VILABU VYOTE VIWILI VINAMAKOSA. UKWELI NI KWAMBA MCHEZAJI NI MALI YA AZAM KWA SABABU WALIMPELEKA SIMBA KWA MKOPO, HILO LIPO WAZI.LAKINI MKOPO HUO ULIKUWA WA MAKUBALIANO MAALUMU KATI YA SIMBA NA AZAM.AZAM WALIMTOA NGASA KWA MUDA WA MWAKA MMOJA.LAKINI AZAM HAWANA HAKI YA KUMUUZA NGASA CLUB NYINGINE BILA KUKAA CHINI NA SIMBA KWANI SIMBA WALISHATOA PESA HIYO KWA MAKUBALIANO YA KUMTUMIA KWA MUDA WA MWAKA MMOJA.ILITAKIWA AZAM WARUDI KWANZA SIMBA KUSITISHA MKOPO HUO ILI WAMUUZE CLUB NYINGINE KWANI SHERIA INARUHUSU.LAKINI AZAM KUAMUA KUMUUZA NGASA BILA KURUDI KWANZA SIMBA KUKUBALIANA HAPO WAMEKOSEA.
    KWA UPANDE WA SIMBA WAO WALISHAKOSEA TANGU MWANZO WA MAKUBALIANO.KWANI HAWAKUPASWA KUMUONGEZEA MKATABA NGASA WAKATI BADO ANAMKATABA NA AZAM.

    USHAURI.
    1.VILABU HIVI VIKAE PAMOJA NA KUKUBALIANA NA WAACHANE NA SIASA ZA MPIRA.WAMUANGALIE NGASA KWA MUSTAKABALI WA MAISHA YAKE,NA UMUHIMU WAKE KATIKA TIMU YA TAIFA.
    2.SIMBA WALEGEZE KAMBA KUHUSU HILI, WAKUBALI KURUDISHIWA PESA YAO ILI WASIPOTEZE MUDA KAMA WALIVYOPOTEZA KATIKA SUALA LA MBUYU TWITE.WAFANYE MAAMUZI YA HARAKA NA KUZIBA PENGO LA NGASA NA KUACHANA NA MALUMBANO KWANI YANAWAVUNJIA HESHIMA VIONGOZI

    ReplyDelete
  32. rage mzee wa sheria ngasa ana mkataba na azam wa mwaka mmoja ni sahihi kuingia nae mkataba nje ya makubaliano na azam ? napokukopesha kitu mda wowote naweza kukitaka ndo maana maliki ndaule ma omary mtaki wamerudi toka lyon na mtibwa.na hiyo dili hata rage nae anajua kuwa ilkuwa kwa mkopo na iltangazwa kwenye radio au wamwekee clips clips za kahemele asikilize.hii sio fat mheshimiwa

    ReplyDelete
  33. Tatizo la Simba ni kwamba walikuwa wanaturidhisha sisi mashabiki, kama waliingia makubaliano ya kupewa mchezaji kwa mkopo kwa nini waingie gharama zote hizo za kununua magari kwa mali ya timu nyingine? mchezaji wa mkopo ni mali ya timu yenye mkataba nae na timu mama inaweza kumuita wakati wowote ndani ya kipindi cha usajili. na ndio walivyofanya Azam, wamemuuza Ngassa katika kipindi cha usajili, na wameahidi kurejesha fedha walizochukua simba (by the way - hawakupaswa kuchukua fedha simba, sijui kwa nini viongozi wa Simba walikuwa wajinga kiasi hiki)!

    ReplyDelete
  34. Nashindwa kuelewa katika soka la bongo hii inakuwaje,lkn ulaya mchezaji akitolewa kwa mkopo anaweza kurudishwa ktk klabu yake baada ya nusu ya muda wa mkataba.ie kama alitolewa july ikifika dec klabu yake inaweza kumrudisha ni kawaida,sjui simba na azam walikuwa na makubaliano gani ya mkopo kwa sababu bongo taratibu sio lazima zifuatwe mizengwe ndio inatumika kuongoza soka.

    ReplyDelete
  35. Cha msingi hapo ni kurudi kwenye mkataba tu,kiukweli Ngasa ni mchezaji halali wa Azam,lakini alienda simba kwa mkopo wa mwaka mmoja. Je katika huo mkataba wa mkopo kuna kipengele kinachowaruhusu Azam kumuuza Ngasa kabla ya muda wa mkopo kuisha? Je kwenye mkataba wa mkopo kuna kipengele kinasema Simba wamzuie Ngasa asiuzwe katikati ya muda wa mkopo? Kama vipengele hivyo havipo basi hilo ni swala la Simba na Azam kukaa pamoja na kujadiliana jinsi ya kumuuza Ngasa katikati ya mkopo lakini sio klabu moja ijione ina haki kuliko nyingine.Kama Azam atalazimisha basi asubiri muda wa mkopo uishe ndio amuuze.Na huo mkataba ambao Simba wanasema waliingia na Ngasa mimi naona huo ni feki na sidhani kama upo TFF.Mkataba halali ni ule ambao uliwasilishwa TFF na sio ambao upo kwenye ofisi za klabu au kwa mtu binafsi.SIMBA NA AZAM KAENI MEZA MOJA MZUNGUMZE KIJANA AENDE SUDAN.

    ReplyDelete