Search This Blog

Saturday, May 19, 2012

REDONDO NA CHUJI WAZUNGUMZIA PATRICK MAFISANGO

Kiungo wa Azam, Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema kifo cha Patrick Mafisango ni pigo kubwa kwake kutokana ndiye alimtaka aondoke Maisha Club ili akalale muda mfupi kabla ya kifo chake.

Redondo aliyekuwa na marehemu Mafisango kwenye ukumbi wa Maisha Club hadi saa 7 usiku ambako Mafisango alimtaka aondoke kwa madai kuwa muda ulikuwa umekwisha.

Akizungumza kwa shida kutokana na kuelemewa na uzito wa msiba huo alisema haelewi ni nini kimetokea na kwa nini alimfukuza pengine wangekuwa wote kwenye safari ya kurudi.

"Tulikuwa wote hadi mwisho kwenye ukumbi wa maisha klabu, lakini ilipofika muda ya saa saba nane kasorobo  Mafisango alinifukuza na kunichukulia taxi nirudi nyumbani na kuniaambia muda umeisha yeye atarudi na jamaa zake ambao alikuwa nao akiwemo mtoto wa dada yake,"alisema na kuongeza

"Nilikubali nikaondoka cha kushangaza napata taarifa alfajiri kuwa Mafisango amefariki Mungu amefanya kazi yake kumchukua, lakini mimi imeniathiri kutokana na mambo mengi niliyoongea nae"alisema na kushindwa kuendelea kuongea.

ATHUMANI IDD CHUJI

"Unafahamu wapo wachezaji wengi wa kigeni wanaocheza soka nchini na waliowahi kucheza soka nchini na kuondoka, lakini sikuwahi akuona mchezaji wa kigeni aliyekuwa akipendwa na wachezaji kama yeye,"alisema Chuji.

Alisema," Mafisango alipendwa na wachezaji wa timu tofauti za Ligi Kuu hasa walipokutana naye nje ya uwanja, alikuwa anapenda kuishi maisha ya kawaida tu na wachezaji wengi walikuwa wakimchukulia kama Mtanzania ila lafudhi yake tu.

No comments:

Post a Comment