Search This Blog

Friday, May 18, 2012

MASIKINI BOBAN: KIFO CHA MAFISANGO KIMEMUUMIZA MNO - WALIKUWA MARAFIKI WAKUBWA SANA.

Haruna Moshi Boban akiwa mwenye huzuni mkubwa leo wakati wa kuaga mwili wa Mafisango. Pole Boban mwenyezi mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu. (Picha kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com/)

Pamoja na kuwa ni wengi tumeumizwa na msiba wa aliyekuwa kiungo wa timu ya Simba Patrick Mafisango Mutesa, lakini ni dhahiri wachezaji wenzie wa Simba wameumizwa zaidi hasa rafiki yake kipenzi Haruna Moshi Boban.
Haruna Moshi Boban akiwa na huzuni tele leo hii wakati wa kumuaga Patrick Mafisango.

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba kwa takribani masaa 24 tangu kifo cha Mafisango kitokee Haruna Moshi ambaye wengi wetu tunamjua kama kama nunda na mtu mwenye aibu sana lakini kufuatia msiba huu wa Mafisango, Boban amekuwa mtu mwenye huzuni sana kiasi cha kushindwa hata kula. 
Emmanuel Okwi akiaga mwili wa Patrick Mafisango.
"Kiukweli msiba wa mwenzetu umetumuumiza sana, lakini Haruna umemuuma zaidi kwa kuwa Mafisango ndio alikuwa rafiki yake mkubwa kuliko wachezaji wote ndani ya Simba. Mafisango na Boban pale Simba walikuwa kama mapacha, yaani muda wote hata tukiwa kambini utawakuta pamoja. Kwa mfano hata tukiwa tumeenda safari kwa ajili ya mechi mara zote wenyewe walikuwa wakilala pamoja, kiukweli walikuwa wakipendana sana na ndioa maana haishangazi kumuona Boban kwenye hali ile." - alikaririwa akisema Emmanuel Okwi kupitia mawasiliano ya mtandao wa BBM.

No comments:

Post a Comment