Search This Blog

Friday, April 19, 2013

EXCLUSIVE: HARUNA NIYONZIMA AFANYIWA UPASUAJI LEO HII


Kiungo mahiri wa Yanga, Haruna Niyonzima leo Ijumaa amefanyiwa upasuaji wa kipele kwenye pua yake ingawa daktari wa timu hiyo Nassoro Matuzya amesema hauweza kuathiri utendaji wake wa kazi.
Matuzya alisema jijini Dar es Salaam kuwa kiungo huyo alifanya mazoezi asubuhi na wenzake, lakini baadaye alimtaka kwenda kujiandaa kwa ajili ya upasuaji huo mdogo.
"Ni kweli leo asubuhi Haruna (Niyonzima) tumemfanyia upasuaji mdogo wa kipele kwenye pua yake katika hospitali ya Mwananyamala."
"Kipele hicho kilimtokea kwenye pua yake. Hakikuwa sehemu nzuri, kwa hiyo tumelazimika kumfanyia upasuaji huo mdogo."
"Kidonda hicho hakiwezi kuathiri utendaji wake wa kazi. Kesho (leo) ataendelea na mazoezi kama kawaida na wenzake kujiwinda na mchezo wa JKT Ruvu." alisema Matuzya.
Alisema kidonda cha upasuaji huo kitakuwa kimepona mara baada ya saa 48 ambazo ni sawa na siku mbili.
"Hadi kufika Jumapili atakuwa hana tatizo lolote. Nafikiri suala la kucheza linabaki kwa mwalimu wa timu." alisema daktari huyo

4 comments:

  1. Duuuuuh! Exclusive yako imenitia presha sana kaka, pole sana kiungo bora kabisa katika ukanda huu wa afrika mashariki na kati, upone haraka iwezekanavyo fundi!

    ReplyDelete
  2. Watu watatia kipepsi hapo patarudi upya.

    ReplyDelete
  3. tishaaaaa sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.duu

    ReplyDelete