Search This Blog

Friday, April 19, 2013

ROONEY NA NAFASI YA KIUNGO NI SAHIHI?? MECHI DHIDI YA WEST HAM ALIPIGA PASI MOJA TU NDANI YA ENEO LA HATARI LA WAPINZANI



Wayne Rooney ni mshambuliaji au kiungo ndani ya kikos cha Manchester United siku hizi za hivi karibuni? 

Wengine wanasema ikiwa Rooney anataka kuendelea kuwa na nafasi ya kikosi cha kwanza ndani ya United inabidi arudi kucheza kwenye kiungo akiziba nafasi ya Paul Scholes kama ambavyo amekuwa akicheza kwenye michezo miwili iliyopita.

Huku wengine wakisema ikiwa United wameamua kufikia maamuzi ya kumuondoa kwenye jukumu la ufungaji basi siku zake ndani ya Old Trafford zinahesabika.

Vyovyote ilivyo - wakati mshambuliaji chaguo la kwanza la England amepiga pasi moja iliyoingia ndani ya eneo la hatari la wapinzani - kama ambavyo Rooney alifanya usiku wa juzi pale Upton Park - unaanza kupata shaka kwamba kuna kitu kisicho sawa.


Wayne Rooney touch map vs West Ham




Michael Carrick touch map vs West Ham
Picha hizi zinaonyesha movements zote na pasi alizotoa Wayne Rooney kwenye mchezo dhidi ya West Ham.

Alicheza vizuri sana dhidi ya Stoke jumapili iliyopita wakati Sir Alex Ferguson alipomchezesha nafasi ya kiungo. Lakini akaheza ovyo dhidi ya West Ham na kutolewa dakika 71 kumpisha Giggs United wakiwa nyuma kwa bao 2-1. 

Kama inavyoonekana kwenye picha Rooney akicheza kwenye kiungo anakuwa anarudi sana nyuma kwenye kukaba hivyo anakuwa hana tishio kwenye ushambuliaji - hapa kwenye picha ya chinitakwimu  zinayoonyesha namna Micheal Carrick ambaye anacheza nyuma zaidi yake alivyokuwa amepenyeza mipira mingi kwenye lango la wapinzani kuliko Rooney ambaye yeye alicheza juu.
 

No comments:

Post a Comment