Search This Blog

Tuesday, January 3, 2012

BECKHAM NJIANI KUBAKI GALAXY - PSG WATHIBITISHA HATOJIUNGA NAO


Paris Saint Germain wamethibitisha David Beckham hatojiunga na timu hiyo.

Mkurugenzi wa ufundi Leornardo amekuwa akijaribu kwa muda mrefu kumsaini ex-England captain baada ya kumalizika kwa mkataba wake na LA Galaxy mwezi November 2011.

Lakini pamoja na kupewa ofa nzuri, Beckham, 36, aliamua kutokwenda Ufaransa kwasababu halikuwa chaguo zuri kwake na familia yake.

Na inaonekana Beckham ataongeza mkataba mpya na LA Galaxy baada ya kumkubalia kucheza katika michuano ya Olympics in summer 2012.

Leonardo alisema: “It’s over, Beckham hatokuja PSG. Inasikitisha lakini kwa sababu ya familia yake iliyopo Los Angeles, ameamua kutokubadilisha kila kitu katika maisha yake.”

Mapema wiki hii Leornardo alikiri nafasi ya PSG kumsaini Beckham ilikuwa ndogo sana.

Alisema: “Tatizo halikuwa la kikazi bali familia yake. Ni vigumu kuchagua kuileta familia yake Paris. Ni chaguo binafsi na rahisi kwake. Namjua Beckham. Nina imani kubwa kwake kama mchezaji na kama Baba. Nafahamu ni uamuzi mgumu kwake kuhama.

No comments:

Post a Comment