Search This Blog

Wednesday, January 4, 2012

ZAKI NA MIDO WATAJWA KATIKA KIKOSI KICHAJO KUPAMBANANA YANGA



Klabu ya Zamalek ya Misri imewasilisha orodha ya wachezaji 26 ambao wamesajiliwa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

Zamalek ambayo imepangwa kucheza na Yanga ya Dar es Salaam raundi ya awali ya michuano hiyo , ina historia ya kulitwaa taji hilo mara tano mpaka mwaka 2002, lakini tangu imekuwa ikihangaika kurejesha ufalme huo, huku wapinzani wao wakubwa Ahly wakiwapiku kwa kulitwaa taji hilo mara sita mwaka 2008.

Ili kuhakikisha wanarejesha utawala wao kwenye soka la Afrika , Zamalek imefanya usajili wa nyota kadhaa ili kuimarisha kikosi chao na katika orodha hiyo ya wachezaji wamo Ahmed Hossam "Mido” na Amri Zaki, ambao hapo kabla walikuwa wakichezea klabu za Ligi Kuu ya England.

Zaki ambaye Julai 22 mwaka 2008, alimaliza mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu ya Ligi Kuu ya England ya Wigan Athletic, ambako alikuwa akilipwa pauni milioni 1.5, pia amewahi kuichezea kwa mkopo Hull City, alijiunga na Zamalek Januari 17 mwaka 2010.

Alitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kwa kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao matatu katika mechi nne za mwanzo alizochezea timu hiyo , mbali na sifa hiyo pia ni

mchezaji anayejulikana kutokana na umahiri wa kupiga mipira vichwa pamoja na kuwa miongoni mwa wafungaji hodari barani Afrika.

Mshambuliaji mwenzake ‘Mido’ aliwahi kuichezea Ajax ya Uholanzi mwaka 2001, ambako baadaye aliondoka na kujiunga na Celta Vigo kwa mkopo mwaka 2003 kabla ya kwenda

Marseille ya Ufaransa ambako nako aliondoka na kujiunga na Roma ya Italia mwaka 2004.

Baada ya hapo alijiunga na Tottenham Hotspurs ya England kwa mkataba wa mkopo wa miezi 18 mwaka 2005 na mwaka uliofuata alipewa mkataba wa kudumu.

Aliondoka Spurs mwaka 2007 akijiunga na Middlesbrough ambako nako hakukaa akijiunga na Wigan Athletic na baadaye West Ham alikokwenda kwa mkopo na alirudi tena Ajax mwaka 2010 ambako klabu hiyo ilikubaliana kuvunja mkataba na mchezaji huyo Januari 4 mwaka huo ndipo alirejea, Zamalek.

Kwa mujibu wa mtandao wa Zamalek hiki ndicho kikosi kamili cha timu hiyo kilichowasilishwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya michuano hiyo ni Abdul-Wahed Al- Sayed - Mahmoud Abdul-Rahim "Jnc", Mahmoud Fathallah, Hany Said, Salah Suleiman, Karim Hassan na Mohamed Abdel Shafi.

Wengine ni Ahmed Samir, Omar Jaber, Hazem Imam, Ibrahim Salah, Merghany Ahmad, Ahmad Tawfiq, Ahmed Hassan, Alaa Ali, Mohammed Saeed, Shikabala, Ahmed Jaffar,

Hamdy Hussein , Ahmed Hossam "Mido", Amr Zaki, Razak Ahmed, Abdel-Kader, Mohammed Ibrahim na Hossam Arafat.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Cafa Yanga itawakaribisha Zamalek katika raundi ya awali ya michuano hiyo kati ya Februari 17 au 19 jijini Dar es Salaam na mchezo wa marudiano utafanyika Machi 2 au 4 jijini Cairo..”

No comments:

Post a Comment