Search This Blog

Friday, January 6, 2012

SIR ALEX FERGUSON - CHELSEA HAWAWEZI KUTUUZIA LAMPARD


Sir Alex Ferguson amesema Manchester United hatoweza kumsajili Frank Lampard kutoka Chelsea.

Mtandao wa Sportsmail wa Uingereza jana wali-reveal kwamba Ferguson alikuwa anafikiria kumsaini kiungo huyo wa kiingereza ambaye siku hizi karibuni amekuwa akipata nafasi chache za kuitumikia Chelsea.

Na inaeleweka kwamba Lampard isingekuwa vigumu sana kwa Lampard kuhamia United akizingatia na nafasi anayopewa na AVB ndani ya The Blues.

Akiongea leo Ijumaa asubuhi, Fergie alisema: “Huwezi kuniambia Chelsea watamuuza Frank Lampard kwa Manchester United in January. Unaamini kweli hilo linawezekana? Chelsea ni kama sisi, kuna kitu wanataka kufanya. Jambo la pili katika hii nusu ya pili ya msimu ni muhimu sana kwao. Kama watajaribu na kutaka kushinda ligi wanahitaji kuwa na wachezaji wao wote bora.

“Nimeshasema ni wachezaji wa namna gani tunaweza kuwasajili mwezi January, ni wachezaji ambao wapo available ambao ni top class players, ambao sio rahisi kuwapata katika dirisha dogo la usajili.

“Unafanyaje? Unamsajili second-rate player? Hapana. Of course huwezi. Majeruhi yanayowakabili wachezaji wetu kipindi hiki yamefanya mashabiki wetu waanze kupiga kelele wakitaka tusajili.

“Ni bora niendelee kuwa na wachezaji hawa nilionao kuliko kumsajili mchezaji ambaye hatopata nafasi hata ya kucheza mchezo mmoja.”

No comments:

Post a Comment