Search This Blog

Thursday, October 4, 2012

DAR- PACHA IMEIONYESHA DUNIA MSISIMKO WA SOKA NCHINI TANZANIA - HUKU REFA AKITIA AIBU

 






.Wachezaji walishindwa kutambua umuhimu wa mchezo huo
. Mwamuzi alikuwa zaidi ya ‘kituko’
.Kwa nini Haruna Moshi na Mwasika walimaliza mchezo?
Mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000 timu za soka za Yanga na Simba zilicheza soka la ‘aibu’ uku wakionekana kama vile wanacheza mchezo wa ‘rugby’.
Baada ya penati iliyopigwa na mshambuliaji Said Bahanuzi kuipatia Yanga bao la kusawazisha mwishoni mwa kipindi cha pili, kiujumla timu hizo ambazo zinachukuliwa kama kioo cha soka la bongo hazikuonesha soka lolote zaidi ya kucheza kibabe na kukamiana tu.
Upande wa pili mwamuzi alishindwa kuyatolea adhabu sahihi baadhi ya matukio makubwa kwenye mchezo huo, Haruna Moshi aliyeingia  dakika 20 za mwisho alistahili kuonyeshwa  kadi nyekundu, alimrukia kwa makusudi beki wa Yanga, Kelvin Yondan na ni dhahiri alitaka kumvunja. Ni aibu ambayo dunia imeishuhudia, lakini tumepata fursa nzuri ya kutangaza ‘msisimko’ uliopo katika mpira wetu kutoka kwa mashabiki.
                 HALI YA MCHEZO ILIVYOKUWA.
Simba walianza mchezo kwa kasi ambayo ilikuwa ikiongezeka kadri dakika zilivyokuwa zikisonga mbele, na dakika ya kwanza tu wakafika katika lango la kipa Yaw Berko, halikuwa shambulizi kubwa lakini lilionyesha kitu kutoka kwa timu hiyo ambayo iliwaanzisha makinda Edward Christopher, Jonas Mkude, Paul Ngalema na Shomari Kapombe katika kikosi chao cha kwanza.
Wakicheza zaidi kwa kutumia upande wa kulia kwa Nassoro Chollo, Simba iliweza kutengeneza bao la kuongoza na bao lao pekee katika mchezo huo baada ya Mwinyi Kazimoto  kupiga krosi ambayo ilimkuta kiungo, Amri Kiemba na kupiga shuti la kiufundi upande wa juu kushoto kwa kipa Berko ndani ya dakika tano Simba wakawa mbele kwa bao 1-0.
Goli La Simba
Mkude ambaye alicheza kama kiungo namba moja wa ulinzi akisaidiwa na Kiemba aliweza kuituliza timu hata pale Yanga walipotaka kupitisha mipira  mirefu, alikimbia kila eneo ambalo alikuwepo mshambuliaji namba mbili wa Yanga, Nizar Khalfan na pia alikuwa akitazama kila eneo ambalo alikuwa akitengeneza nafasi, akamzima Nizar naye akawa bora ndani ya eneo la pili la uwanja kutoka golini kwake, aliwalinda vizuri Juma Nyosso na Kapombe na hata pale alipokuwa akipanda kusaidia mashambulizi alitazama usalama kwanza, ndiye aliyemfanya Kiemba kusogea kwa uhuru katika eneo la hatari la Yanga na kufunga.
 Wakati Fulani Haruna Niyonzima alihitaji kucheza nje ya nafasi yake ili kuhakikisha, Mkude hasogei katika eneo lao la hatari na hapo ndipo zikaja dakika 45 ngumu za Athuman Idd ‘Chuji’ ambaye pamoja na kutambua alikuwa na jukumu la kumzima Mwinyi Kazimoto lakini akajikuta akiingiziwa mzigo mwingine wa kumkabili Kiemba pia.

 Msuva na Hamis Kiiza ambao walianza pamoja na Bahanunzi na Nizar katika safu ya mashambulizi hawakuwa na msaada wakati timu yao ‘ikipepesuka uwanjani’, walikufa na kutoa nafasi ya Simba kutawala mchezo kwa dakika 30 za kwanza. Kocha wa Yanga, Ernest Brandts alipoona Simba wametawala eneo la kati  aliamua kumtoa mshambuliaji Hamis Kizza dakika ya 37 na kumuingiza kiungo Frank Domayo ili kwenda kuongeza utulivu pamoja ubunifu wa kupitisha pasi za kupenyeza katika eneo la hatari la Simba ambayo ilioneka kuzidiwa kiasi katika robo ya mwisho ya kipichi cha kwanza.
 Simba wakaendelea kukaza hadi mapumziko wakawa mbele kwa bao 1-0.
             KITU KIPYA NA KILICHOVUTIA KATIKA NUSU YA KWANZA
Mbuyu Twite alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa ‘DAR-PACHA’ na hakika aliweza kutimiza vyema jukumu la beki namba mbili, alikuwa anahitaji kujibadilisha kutoka mchezaji wa ‘ridhaa’ haki kuwa mchezaji wa kimataifa mara mbili tu baada ya kumkabili kinda Edward Christopher. EDO alikuwa mchezaji mdogo zaidi katika mchezo huo na ilikuwa ni mara yake ya kwanza pia kucheza mechi ya mahasimu wa soka la bongo.
Wakati, Twite akimtazama, Edo  kabla ya mchezo kuanza bila shaka alikuwa akichekea moyoni na kusema ‘ duh, sasa Simba wameniletea aka katoto badala ya…..’ lakini mara baada ya mchezo kuanza Simba wakaamua ‘kutest’ upande wa Twite, kila mpira akawa anapelekewa Edo na na baada ya kufanywa hivyo mara tatu refarii alionekana kuwabeba Yanga kwa kushindwa kutoa penati baada ya Nadir Harooub kumchezea rafu Edo ndani ya eneo la hatari baada ya Edo kumuadaa Twite. Hapo Twite akatambua thamani yake mbele ya mashabiki wa Yanga, akajitoa katika uchezaji wa ridhaa na kuwa mchezaji wa kimataifa na kumzima kabisa kinda huyo, huku yeye akionekana mchezaji tishio zaidi kwa kipa wa Simba, Juma Kaseja kwani mara mbili allipiga mashuti ya mbali na moja akigongesha mlingoti wa juu,Twite Alicheza vizuri na alionyesha namna mchezaji anavyoweza kuendana na watakacho mashabiki na kujibadilisha mchezoni kwa manufaa ya timu.
          KILICHO HARIBU LADHA YA MCHEZO KATIKA KIPINDI CHA KWANZA.
Ernest Brandts alikuwa akiiongoza Yanga kwa mara ya kwanza kama kocha mkuu na amepata matokeo mazuri kiasi.
Lakini aliingiza timu yake uwanjani akiwa na mbinu mbovu. Wakati, Simba ilikuwa na mapengo ya wachezaji wake muhimu kama Amir Maftah na Emmanuel Okwi kutokana na kuwa na adhabu ya kadi na wakikosa huduma waliyotaraji kutoka kwa Haruna Moshi kutokana na kusumbuliwa na  maralia, kocha wa timu hiyo, Milovan Cirkovic aliweza kuingiza machaguo mapya kama Mkude, Ngalema  na EDO huku akijiamini.
Brandts akiwa na washambuliaji wake wote wanne tena wakiwa na afya bora alishindwa kuipanga timu yake katika aina nzuri ya wachezaji ambao wangeweza kucheza mfumo wa 4-3-3 ambao kimsingi timu kama Yanga si rahisi kuumudu, kimazingira na utamaduni. Huu ni mfumo wa Simba lakini bado siyo sababu ya kushindwa kuzaa matunda kama Yanga pia watautumia vizuri.
Kumuanzisha Nizar kama mshambuliaji namba mbili katika mfumo huo ilikuwa ni kosa kubwa, lakini bado alishindwa kutambua umuhimu wa Kizza akicheza kama mshambuliaji namba mbili na Nizar akicheza pembeni, angeweza kuwapanga Kizza na Bahanunzi kama washambuliaji wawili wa kwanza na kumsogeza Nizar eneo la Kati kisha Msuva akacheza kama mshambuliaji wa tatu. Lakini hata kama angewapanga hivi bado asingekuwa na machaguo bora katika mfumo huo. Angewaanzisha, Didier Kavumbangu, Kizza na Bahanunzi na Yanga wangeweza kupata ushindi katika kipindi hiki.
Pia tatizo la wachezaji wetu kukosa nguvu lilionekana dhahiri japo lilizidi zaidi kwa upande wa Yanga, hata Simba hawakuonekana kuwa na nguvu hasa pale walipohitajika kuzitumia katika maeneo muhimu, Ngassa na Edo kwa upande wa Simba walionesha udhaifu huu na hata pasi za viungo Kiemba, Mwinyi na Mkude hazikuwa na nguvu. Tatizo la kupigiana pasi ‘laini’ ni kubwa katika nchi yetu na kama hakutakuwa na mabadiliko bado tutaonekana ni walewale kila siku japo tuna vipaji. Tatizo la kuanguka anguka kwa wachezaji lilipunguza sana radha ya mchezo.
        NYOTA WA KIPINDI HIKI
Paul Ngalema aliingia kikosini baada ya Maftah kuwa na adhabu, lakini aliweza kuonyesha ni kwa nini timu hiyo ya Simba ilimsajili ili kuwa mchezaji ambaye anaweza kuziba pengo lolote pale anapohitajika, Ngalema akicheza mchezo wake wa kwanza mbele ya watazamaji zaidi ya 50,000 aliweza kuonekana  mchezaji anayeupenda zaidi mguu wake wa kushoto, kila alipoenda kukaba alifanikiwa kutibua ‘muvu’ za Yanga, alipopiga pasi basi ilikuwa safi na ilifika alipotaka, mara chache aliweza kuonesha kipaji cha kupiga pasi ndefu japo anahitaji kufanyia mazoezi zaidi. Aliweza kumzima kabisa Msuva na kupelekea ashindwe kusogea katika lango lao, alicheza kama alivyotaka kucheza yeye.
        KIPINDI CHA PILI
Hakikuwa cha ufundi sana, lakini inaonekana Yanga waliingia kwa nia ya kuhitaji kusawazisha zaidi na kupata ushindi kama ingewezekana, waliingia kwa nguvu uku Niyonzima akirejea katika eneo lake la kati kusaidiana na Domayo Yanga wakaanza kupeleka mashambulizi ya kasi lakini bado Juma Kaseja atabaki kipa bora katika historia ya  mchezo wa mahasimu hao, kwani aliweza kuzuia mashuti mengi ambayo yalipigwa na wachezaji wa Yanga. Na alipongia Kavumbangu katika nafasi ya Nizar mara baada ya mapumziko Yanga walionekana wapo vizuri zaidi ya Simba na walihitaji matokeo.
Mpira uliorushwa na Twite unashindwa kuondolewa na Ngalema ambaye anajikuta akiushika na kuwa penalti. Said Bahanunzi alifunga bao lake la kwanza msimu huu katika ligi kuu baada ya kupiga ‘kiki kali ya ufundi’ na kumdanganya kipa Kaseja. Yanga wakasawazisha na hapo ndipo ukaja muda mbaya zaidi katika mchezo huo kwa wachezaji wa timu hizo kuanza kuchezeana rafu zisizo na maana na kupelekea mwamuzi kushindwa kulimudu pambano hilo
Penati ya Saidi Bahanuzi
      KILICHOKERA KATIKA KIPINDI HIKI
Ni mwamuzi Mathew Akrama kushindwa kuwatoa nje kwa kadi nyekundu Haruna Moshi ambaye alitaka kumvunja kabisa Yondani, Haruna alidhamiria kabisa na hata wakati anakimbilia mpira ule alionekana haendi kucheza mpira. Pia alishindwa kutoa kadi nyekundu kwa Athumani Idd Chuji katika dakika ya 94 alipomchezea rafu Akuffor akiwa yeye ndio mchezaji wa Yanga wa mwisho. Pia alishindwa kumuadhibu Mwasika alimpomkanyaga kusudi Mwinyi Kazimoto nje kidogo ya eneo la penati, na hata Mbuyu Twitte alimpovuta Mrisho Ngassa.
Kwa kifupi akaivuruga kabisa mechi ya ikawa mechi ya ‘kipuuzi’ kuanzia kwa wachezaji hadi waamuzi.

3 comments:

  1. Nakubaliana na wewe SD! Mchezo huu ulikuwa unafuatiliwa na watu wengi sana nje ya hao walioingia uwanjani kwani mchezo huo ulikuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha SS9,watu wengi mashabiki na wenye malengo ya kusaka vipaji waliishia kuona "vituko" vya soka la bongo...lakini taratibu tutafika, cha msingi "feedback" kama hizi lazima ziwafikie walengwa (Timu na hasa uongozi) na TFF ili kuwe na mabadiliko kiujumla na hatimaye tuone mapinduzi ya mchezo huu maarufu na unaopendwa na mashabiki wengi kote duniani!

    ReplyDelete
  2. Shafii bila unazi yule dogo Edo ukiangalia replay inaonyesha hakufanyiwa rafu na Cannavaro anaalistahili kadi ya kwa kosa la kutaka kumdanganya refa.
    Ni kweli Moshi, chuji na Mwasika walistahili kadi nyekundu.

    Lakini napenda nimsifu mwamuzi kwa kutokutoa kadi kwani angeharibu radha ya mpira kama tulivyoona mapambano mengine ya mahasimu hao yaliyoharibiwa na maamuzi ya mwamuzi.

    Na wala sipendi kusema mechi ilikuwa mbaya kwani imeeonyesha kuna good kids who are coming kwangu mimi masikitiko yangu kuna wachezaji wakigeni ambao viwango vyao vidogo hizi timu zetu zimewasajili

    ReplyDelete
  3. At least ungetuonyesha number of chances created, who dominated the game and possession, who was technically good sio unakuja na kujaribu kuponda wakati mechi imekwisha na watu walifurahia at least there is a bright future ahead

    ReplyDelete