Search This Blog

Thursday, December 13, 2012

KALI YA LEO: CLAUDIO RANIERI ATISHIA KUWAUA WACHEZAJI WA MAONACO BAADA YA KUFUNGWA


Aibu ya kipigo cha 3-0 dhidi ya Caen imeifanya Monaco kushuka hadi nafasi ya pili katika ligi ya daraja la kwanza nchini Ufaransa na sasa meneja Claudio Ranieri ametangaza kwamba ikiwa wachezaji wake hawatoshinda mechi ijayo, atawaua. Kwa sababu ipi ni njia nzuri ya kuwatia hamasa ya kufanya wachezaji wanaopewa kila kitu lakini wanashindwa kufanya vizuri zaidi ya kuwatishia maisha yao?
Kutoka Reuters:
"Nina hasira sana. Kinguvu tulikuwa wapili kwa ubora na haya ndio matokeo. Nataka kushinda. Inatupasa kushinda vinginevyo nitakuja kuwaua hawa wachezaji," kocha wa zamani wa Chelsea na Juventus, ambaye alijiunga na Monaco mwezi watano, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari siku ya jumatano.
"Timu tunazokutana nazo zinajituma kwa asilimia mia, na wakati sie tukiwa hatufanyi hivyo ni vigumu kushinda."
Hii ndio labda njia sahihi ambayo Arsene Wenger inabidi ajaribu kuitumia.

No comments:

Post a Comment