Search This Blog

Thursday, December 13, 2012

UCHAGUZI WA DRFA: KASONGO MWENYEKITI MPYA - DAUDA NA TEMBELE CHALIII

Uchaguzi wa chama cha mpira jijini Dar es Salaam DRFA umefanyika leo mchana na matokeo yapo kama ifuatavyo: Mwenyekiti ni Almas Kasongo amepata kura 11, akifuatiwa na mpinzani wake Evans Aveva amepata kura 7.                     Makamu m/kiti: Mede Ramadhani ambaye alipata kura 11 na kumfunika vibaya Ally Mayai alyepata kura 3.                                   Mjumbe mkutano mkuu - Muhsin Said aliwashinda wapinzani kwa kura 10, akafuatiwa na Shufaa Jumanne aliyepata 6, huku Shaffih Dauda akiambulia kura 2.                                             Uwakilishi wa vilabu ulienda kwa Benny Kisaka aliyebeba kura 14, na kumzidi mpinzani wake Philemon Ntahilaji aliyepata kura 4.                                                                                                     Katibu Mkuu akachaguliwa kuwa Msanifu Kondo.

















8 comments:

  1. Pole sana kaka ndio hivyo, bado una future nzuri usikate tamaa....naona kura moja ilikuwa yako na maybe nyinginge ya Mayay.....tunataka watu kama nyinyi kwenye mpira, hao wengine wakimbilia huko kwa umaarufu tu.

    ReplyDelete
  2. Like Michael scofield like Shaffih Dauda... The Mission is done....

    ReplyDelete
  3. Shafihh this is what you deserved maana ulitumia nafasi uliyonayo clouds kuchonga sanaaaaaaa dhidi ya wengine ukasahau hao ndio wapiga kura siku ya mwisho na hatimaye wamekutosa laivu. Next time usitukane wakunga na uzazi ungalipo!!!!

    ReplyDelete
  4. Yaani mbona mambo? Shafii, Aibu kubwa. Hivi unatembea mtaani bado? Alafu unasingizia eti Ulitumwa na Takukuru hakuna kitu Kama hicho na hapo utafeli vile vile. Kura mbili? Mamaaaaaa. Pole baba haya sasa yako wapi ya kuwakata wakina mazwile? Limekurudia kwa Aibu. Shuuuuuuu

    ReplyDelete
  5. Imekula kwako Shafii, pole. Usiendelee kuchonga tena kwa kutumia vyombo vya habari utadhani vyako. Unafanya hivyo huku ulimua fika wenzako hawawezi kujitetea redioni Kama wewe. Sasa hushangai? Pamoja na promo yote mbona umepigwa chink? Yaani sipati picha kura mbili? Kweli aibu. Katubu

    ReplyDelete
  6. Alistahili kupigwa chini.

    ReplyDelete
  7. Kama mimi naacha kutangaza

    ReplyDelete