Search This Blog

Saturday, December 15, 2012

CANNAVARO, AGGREY MORRIS , MCHA, NUHU NA WENZAO HATARINI KULETA MGOGORO KATI YA TFF NA ZFA

Kikao cha Kamati Tendaji cha ZFA Taifa, kilichokutana jana kwa ajili ya kujadili tukio la utovu wa nidhamu kilichofanywa na wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar cha kuamua kugawa pesa za zawadi ya ushindi ya dola 10,000 walizopewa baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya kombe la chalenji iliyomalizika nchini Uganda, kimeamua kuandika burua kwa TFF kueleza kusikitishwa na hatua ya TFF ya kutowaondoa katika timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wachezaji wa Zanzibar ambao wamesimamishwa kucheza soka ndani na nje yanchi.

Akizungumza jana mara baada ya kumaliza kwa kikao cha kamati tendaji cha ZFA Taifa, mjumbe wa kamati tendaji ambaye ni mwanasheria wa Zfa, Abdallah Juma, amesema kitendo cha TFF kuendelea kuwaruhusu wachezaji hao kufanya mazoezi na Timu ya Taifa ni dharau kwa ZFA ambao katika barua ya iliyoandikwa tarehe 11.12.2012 ikiwa na kumbukumbu namba
Ref.ZFA/1/2012 kwenda kwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ililitaka Shirikisho hilo kuwaondosha mara moja kwenye timu hiyo, mpaka pale Zfa watakapotoa taarifa nyengine.


Hata hivyo Akizungumza juzi, ofisa habari wa TFF Boniface Wambura, alisema kuwa barua hiyo haikuwataka kuwaondoa wachezaji hao kwa vile tu wamesimamishwa na sio kufungiwa.


Wachezaji ambao Zfa imetaka waondolewe katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ni:

1. Mwadini Ali -  Azam Sport Club
2. Agrey Moris -   Azam Sport Club
3. Samir Haji Nuhu -Azam Sport Club
4. Khamis Mcha - Azam Sport Club
5. Nassor Masoud - Simba Sport Club
6. Nadir Haruob - Young Football Team
7. Twaha Mohamed- Mtibwa Sport Club
8. Suleiman Kassim - Coastal Union
9. Amir Hamad - JKT Oljoro
10. Abdulghan Gulam -African Lyon 

Hata hivyo kikao hicho kilichokaa jana mchana kimeshindwa kuangaza adhabu watakazozitoa kwa wachezaji hao mpaka watakapopata baraka kutoka Serikalini.

Wakati huo huo orodha ya wachezaji waliorejesha fedha imeongezeka na mpaka jana jumla ya wachezaji 12 wamerejesha fedha hizo.

1 comment:

  1. hii nidhahiri ZFA walitaka kuwadhulumu wachezaji haki yao nao wakajiwahi sababu ZFA hawaelezi hizo fedha zingegawiwa vipi kama wasingegawana wenyewe badala yake wanatakawarejeshewe zote utafikiri wachezaji hawakuwa na chao hapo. Acha dhuluma ZFA.

    ReplyDelete