Search This Blog

Friday, December 14, 2012

SPORTS XTRA& BAR WADHAMINI KOZI YA WAAMUZI WA SOKA MKOA WA DAR ES SALAAM!

Alex Luambano akimkabidhi mratibu wa kozi ya waamuzi wa soka mkoa wa Dar Es Salaam mwamuzi Hashim Ramadhani, Chama cha waamuzi cha manispaa ya Kinondoni ( KIFRA ) Kimeandaa kozi ya kuwaongezea ujuzi waaamuzi wa mpira wa miguu wa mkoa wa Dar Es Salaam inayotaraji kufanyika hivi karibuni huko Bagamoyo.
Kitengo cha michezo cha CLOUDS MEDIA GROUP kimetoa udhamini wa SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI MOJA.

'' Sisi kama idara tumekuwa mbele kupigania maendeleo ya michezo hapa nchini hasa mchezo wa soka kwaiyo walipokuja waamuzi kuomba tuwasaidie kufanikisha kozi yao tukaona ni jambo la msingi,basi kama idara tukawachangia sehemu ya bajeti kiasi cha shilingi 1,000,000/= alisema Alex Luambano mmoja wa watangazi wa vipindi vya michezo vya SPORTS XTRA na SPORTS BAR.

2 comments:

  1. Nawapongeza kwa kuonesha moyo wa uzalendo,,kazi na dawa,mnawachana kisha mnawasaidia kuonesha kwamba mnachokisema c chuki bali ni kwa maendeleo ya taifa..

    ReplyDelete
  2. Nawapongeza sana clouds media group kwa hilo naamin hiyo kozi itakuwa chachu yakutupatia waamuzi bora nchini

    ReplyDelete