Search This Blog

Thursday, December 13, 2012

OFFICIAL: MILOVAN APIGWA CHINI SIMBA - HUYU NDIO KOCHA MPYA - ZISOME SIFA NA TAKWIMU ZAK




Klabu ya ya Simba SC jana ilitangaza rasmi kwamba imevunja mkataba na kocha Mserbia Milovan Cirkovic na kutangza kumleta kocha mpya kutoka nchini Ufaransa Patrick Liewig.

Akizungumza jana na waandishi wa habari afisa habari a Simba Ezekiel Kamwaga alisema wameamua kumchukua Liewig kwa sababu ni kocha anayendana na falasafa ya Simba na hali ya soka la Tanzania lilivyo sasa.

Kocha huyo ambaye amewahi kuvifundisha vilabu vingi katika ulimwengu wa soka vikiwemo PSG ya Ufaransa alipokuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo huku akihusika zaidi na academy ya timu hiyo, Club African ya Tunisia pamoja moja klabu kubwa barani Afrika ya ASEC Mimosas ya Cote d'Ivoire.

Liewig ambaye ni mtalaam aliyebobea katika soka la vijana anategemewa kutua Tanzania ndani ya kipindi cha wiki mbili mpaka tatu zijazo kupisha msimu wa sikukuu ya krisimasi.  

HUU NDIO WASIFU WA KOCHA MPYA WA SIMBA 
 

15 comments:

  1. Tatizo la Simba sio la kocha ni la uongozi kwa hiyo bila kutatua tatizo hilo sidhani hata akija Sir Alex kama atafanya lolote. Pili, kuna mashindano ya club bingwa ya Africa mapema mwakani wakati huo huenda kocha mpya atakuwa ndio anamalizia process ya kuanza ajira, viongozi wa Simba mnategemea nini au mmekwishaamua kutolewa mapema ili kocha mpya aanze upya?

    ReplyDelete
  2. Tatizo siyo kocha, ni fitina za viongozi wetu. Haiwezekani makocha wote wanaopitia kwenye hizi timu zetu wawe hawafai.
    Huyu naye atatimuliwa tu, ngoja wafungwe na kulwa mara 2 tu.

    ReplyDelete
  3. Baba karibu Tanzania waswaili wanasema "MGENI AJE MWENYEJI APONE".Ushauri wa bure kwa wanachama wa simba mpeni muda kocha sio mechi moja tu munamfukuza hiyo sio kazi.

    ReplyDelete
  4. cdhani kama itakuwa mwarobain

    ReplyDelete
  5. Simba acheni mambo yenu Hayo ya Kijinga,Milovani Mtamkumbuka sana ni kocha mzuri kuliko hata huyo mliye mleta shauli yenu Yanga itawaumiza.

    ReplyDelete
  6. wanasimba tuwe tunawapa makocha wetu mda wa kutosha. tuabadilisha mpaka lini? yaseer ammour kutoka moshi.

    ReplyDelete
  7. Shaffih hao kina Rage wanaleta siasa kwenye soka. Nadhani imefika wkt wanasiasa wabaki kwenye siasa wawaachie watu wa mpira washughulike na mpira wao. Mipango ya kisiasa kwenye soka tumechoka nayo. Club hz haziwezi kufika mbali kwa aina ya viongozi tulionao. Watueleze uwanja wamefikia hatua gan? Sio mambo ya mwalimu.

    ReplyDelete
  8. CV. haitofatiani na ya MILOVAN si mwarobaini kwa simba mipango ya timu na malengo ya baadae kwa timu ndio msingi na si CV ZA MAKOCHA HATA PHIRI PARTRICK CV YAKE BOMBA KWELI LAKINI HAYUPO

    ReplyDelete
  9. tutoe muda kwa mwalim mpya na vilevile tuwekeze kwenye soka la vijana ili tuachane na migogoro ya kugombea wachezaji na vijana ambao tumewalea kwa miaka mingi tuwape nafasi waonekane.

    ReplyDelete
  10. mamaaaaaaaaaa,wamebugi.prof. kapigwa chini hawajui kuwa tatizo si kocha.Kwa heri simba.Kocha mwenyewe anafunikwa ile kali na Brandts.

    ReplyDelete
  11. Kila mtu ana mawazo yake, lakini mimi bado naona Milovan ana nafasi kubwa sana ndani ya Simba, labda kama kuna jambo ambalo sisi tulioko nje hatuwezi kuliona au kulijua zaidi ya viongozi!Anyways, tusubiri tuone!
    Pia viongozi wa hizi timu mbili jaribuni kubadilika, kwani mara nyingi maamuzi yenu yanatuumiza sana sisi mashabiki, ikichangiwa na msimamizi wenu ( TFF ) nao kama "wamekatwa kichwa".
    Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  12. simba na yanga hawana hata viwanja vyinavyofaa kwa ajili ya mazoezi...makocha ndio maana wanashindwa kufikisha ujumbe wanaotaka kwa wachezaji na kuishia kuwafukuza makocha badala ya kuwatafutia viwanja

    ReplyDelete
  13. Kikristo (english) tatizo,je hicho kifaransa tutaelewa?TAFAKARI.

    ReplyDelete
  14. moja ya uamuzi mbovu ambao hauna msing wowote, haiwezekani uongozi ugombane halafu madhara yahamie kwa kocha.siungi mkono hatua ya uongozi wa klabu yetu ya simba kumfukuza milovan..

    ReplyDelete