Search This Blog

Thursday, February 7, 2013

EXCLUSIVE: NIYONZIMA KAMA YANGA ISIPOTWAA UBINGWA WA LIGI MSIMU NITAONDOKA


KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amefunguka na kusema kama Yanga itashindwa kutwaa taji la ligi msimu huu ataachana na timu hiyo.
Mnyarwanda huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa alijiwekea malengo yake kabla ya kutua ya Yanga, hivyo kama atashindwa kuyatimiza ataondoka na kutafuta maisha katika klabu nyingine nje ya nchi.
"Kuna malengo ambayo nilijiwekea kabla ya kuja Yanga. Nikuhakikisha tunashinda kila Kombe ambalo tunashiriki."
Alisema anaweza kujivunia kutwaa Kombe la Kagame mwaka jana na Yanga, lakini kwa sasa anafikiri ni wakati mwafaka kwake kubeba taji la Ligi Kuu Bara na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
"Nafikiri kwa sasa tuna timu inayoundwa na wachezaji wazuri na wenye vipaji vikubwa vya soka." alisema Niyonzima.
Aliongeza; "Kama itatokea Yanga imeshindwa kufanya hivyo nitatafuta timu nyingine nje ya nchi kuichezea."
Hata hivyo, Yanga inaweza kumbana nyota huyo kutokana na mkataba wake kumalizika mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment